Header AD

Dawa za Asili 10 zinazotibu chunusi

Chunusi
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni.
Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.
Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.
Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents).

1. Magadi Soda:
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge hicho sehemu iliyoathirika na chunusi.
Kwa muda wa dakika 15 hadi 20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiyo ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapoona athari za chunusi zimepotea.
2. Matango:
Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
Matango ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kisha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Acha likae kwa muda wa dakika 15 hadi 20 hivi, kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu hadi utakapopona.
3. Kitunguu Swaumu:
Unaweza kutumia kitunguu swaumu kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu swaumu huleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bakteria sababu kina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili ya kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili).
Twanga kitungu swaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi huku ukishikilia kwa dakika 5 mpaka 10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya hivyo asubuhi na jioni.
4. Mnanaa (Peppermint):
Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni. Majani ya mnanaa hutumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa.
Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.
5. Limao:
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.
6. Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.
7. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.
8. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanya kazi vizuri.
Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.
9. Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha mpaka asubuhi.
10. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10 hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.
MHIMU: Kunywa maji ya kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe na mazoezi ya viungo na ujiweke msafi kila mara.
Njia hizi za Asili zinaweza kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
Dawa za Asili 10 zinazotibu chunusi Dawa za Asili 10 zinazotibu chunusi Reviewed by crispaseve on 03:23 Rating: 5

No comments

Post AD