UBALOZI WA JAPAN NCHINI WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO MKOANI IRINGA
Balozi
wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa
kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni
Shule ya Idodi sekondari leo
Balozi
wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa
kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni
Shule ya Idodi sekondari leo
Vitanda vilivyopo katika bweni hilo
Hili ndilo bweni la kisasa lililojengwa na ubalozi wa Japan nchini
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkaribisha balozi wa Japan nchini
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akizungumza na wananchi na wanafunzi wa sekondari ya Idodi
Balozi
wa Japan nchini Masaharu Yoshida akikabidhi taa za mionzi ya jua kwa
mkuu wa shule ya sekondari Idodi kulia kwake ni mbunge wa Isiman Wiliam
Lukuvi na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na katibu wa
CCM Iringa vijijini Dodo Sambo
Balozi wa Japan nchini akimkabidhi taa hizo mbunge wa Isimani wiliam Lukuvi
Waziri
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa
Ismani akimsaidia balozi wa Japan nchini kukaa katika kiti cha asili ya
Kihehe baada ya kuvishwa nguo hizo za heshima
Balozi wa Japan nchini akivishwa nguo za kichifu wa wahehe
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akivishwa nguo za kichifu
balozi wa japan nchini akiwa na nguo za kijadi za kihehe akisema hapa KAZI TU
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na waziri Lukuvi na DC Iringa
Kasesela wakiwa na balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida
NA MatukiodaimaBlog
UBALOZI
wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali
ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini
ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt
John Magufuli.
ubalozi
huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule
ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi
milioni 270.
Akizungumza
leo wakati wa uzinduzi wa Bweni hilo la wanafunzi shule ya sekondari ya
Idodi Iringa balozi Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo
inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono
shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.
Alisema
kuwa hatua Japan kufika kusaidia ujenzi wa bweni hilo katika shule ya
sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Ismani
Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
aliloomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali kuteketea kwa
Moto.
"waziri
Lukuvi lileta maombi ya mradi wa kujengewa miradi hiyo ya maendeleo
ambayo ni Hostel ya wasichana shale ya wasichana Ismani ambayo ilijengwa
toka mwaka 2005 na mwaka2008 kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa
katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika
zahanati ya Mlowa... namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi
hiyo"
Balozi
huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi
sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166
sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.
"
Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya
kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji, Hosteli hii sasa inauwezo wa kulaza
wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi ni matumaini yangu mradi huu
utatunzwa vema"
Balozi
huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo
Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu
ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika
bweni hilo.
Hata
hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada
za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema
kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia
kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo
litatunzwa vizuri.
Mbunge
wa Ismani waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa
bweni na miradi mingine bado amepongeza kwa hatua ya balozi huyu
kubariki zaidi ya shilingi milioni 11 zilizobaki katika ujenzi wa bweni
hilo kutumika kununua vifaa vya kusambaza maji ya kisima
kitakachochimbwa shuleni hapo.
UBALOZI WA JAPAN NCHINI WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO MKOANI IRINGA
Reviewed by crispaseve
on
02:28
Rating:
Post a Comment