NEEMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA DAR ES SALAAM
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa
Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa
upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji,
Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha
na kutibu Maji taka.
Makonda
amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni
kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia
Wananchi wote.
Amesema
kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji
wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na
Bunju*vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.
Katika
ziara hiyo pia Makonda ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye
Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa
kuzalisha Lita 16,000 kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa
Wilaya ya Ubungo.
Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo
kutajengwa
Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la
Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu
kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali ya
Japan.
Hata
hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha
Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia
miradi mbalimbali inayoendelea.
Amewataka
Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za
DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo
watawekewa utaratibu wa malipo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama Ujenzi
wa moja ya Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo
yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama mambo ya kupitishia
maji ikiwa ni pia sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake
kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la
Dar
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo mafupi juu ya
muundo mzma mzima wa miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake
kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la
Dar
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama miundo mbinu ya maji
ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya
kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishiriki kuchimba mtaro wa
kupitisha bomba la maji ikiwa ni sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo
kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa
wakazi wa jiji la Dar
NEEMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
11:14
Rating:
Post a Comment