KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA
Kampuni
ya Kilua Industrial Group of Companies imeandaa kongamano kubwa la
uwekezaji wa Viwanda kwa kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya
Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na
makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China.
Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo,Mohamed Said Kilua amesema kuwa kongamano
hilo linatarajia kufanyika Oktoba 25,2017 katika hoteli kubwa yenye
hadhi ya nyota tano jijini Beijing,litakalojumuisha wafanyashabiashara
wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali
nchini China.
“Sisi
Kilua Industrial Group of Companies tumeamua kuibeba dhana ya Tanzania
ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya
Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya
Viwanda, na kwa njia moja ama nyingine iweze kuzigeuza rasimali
maliasili kuwa bidhaa”alisema Kilua.
Tanzania
iliyojaaliwa ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha mazao ya Chakula na
Biashara,haiwezi kutafsiri maendeleo hayo ya Kilimo bila kuzigeuza
bidhaa zilizoandaliwa kwa soko la ndani na lile la Kimataifa bila kuwepo
na viwanda vidogo/vya kati na vikubwa vitakavyozalisha bidhaa zenye
viwango vyenye ubora katika ushindani wa soko”alisisitiza Kilua.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua
Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua (pichani shoto) pamoja
na viongozi waandamizi wa Serikali ya mkoa wa Pwani wakipatiwa
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huateng Metalluargical
Co.Ltd, Chunsheng Jiang (wa nne kulia) kuhusiana na michoro waliyopewa
kama zawadi, ikionesha mandhari ya maeneo mbalimbali ya jiji la Beijing
pamoja na shughuli zao nchini China.
Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina.
Aidha
baada ya kukutana leo viongozi hao pamoja na wadau wakuu wa mambo ya
viwanda nchini China, ambapo Oktoba 25 kutakuwepo na Kongamano
utakaohusu masuala ya viwanda,utakaojumuisha wadau wapatao 200 kutoka
maeneo mbalimbali nchini humo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhina akikata kipande cha
nyama ya Mbuzi,ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha wageni na wenyeji kwenye
chakula cha jioni kiliochoandaliwa na wenyeji wa Beijing,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni Kilua Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kilua,kulia ni Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga wakishuhudia tukio hilo usiku huu.
Baadhi ya wenyeji ambao nao wanatarajiwa kushiriki kongamano la Viwanda
linalotarajia kufanyika Octoba 25,2017 chini ya Uratibu mkubwa wa
kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies,jijini Beijing nchini China chin
Wageni wakiandaliwa chakula jioni
KAMPUNI YA KILUA INDUSTRIAL GROUP YAANDAA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI WA VIWANDA JIJINI BEIJING,NCHINI CHINA
Reviewed by crispaseve
on
03:04
Rating:
Post a Comment