MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi
wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za
serikali za kijiji cha Mtavira.
Na Mathias Canal, Singida
Mwenyekiti
wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka amevuliwa uongozini na
Wananchi Wakati wa Mkutano wa hadhara kutokana na tuhuma za kuruhusu na
kuingiza wavamizi katika hifadhi ya msitu zinazomkabili huku wananchi
hao wakipendekeza Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndg
Mussa Mkumbo kuendelea Kuhudumu katika nafasi hiyo.
Mkutano
huo uliofanyika katika eneo la Ofisi ya Kijiji Cha Mtavira na
kuhudhuriwa na wananchi 353 kutoka Kijiji Cha Makilawa, Mtavira na Mteva
Kata ya Makilawa umepelekea pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira Ndg
Jilala Lutelemula kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili
ikiwemo tuhuma za kuchukua Rushwa ili kuwaacha wafugaji waendelee kuishi
na kuharibu msitu.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi
wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za
serikali za kijiji cha Mtavira.
Mara
Baada ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Aliagiza kuitishwa Mkutano wa
wananchi haraka iwezekanavyo ili kuchagua Mwenyekiti mpya ambapo pia
ameagiza Mwenyekiti huyo kutiwa nguvuni ili kulisaidia Jeshi la polisi
kubaini wahujumu wa msitu huo.
Mhe
Mtaturu pia aliliamuru Jeshi la polisi kumtafuta popote alipo aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka kutokana na tuhuma
zinazomkabili ikiwemo kuzuia wananchi kuhama katika msitu huo Jambo
ambalo Ni kosa kisheria.
Usiku
wa kuamkia Octoba 17, 2017 Mhe Mtaturu aliongoza Kamati ya ulinzi na
usalama Wilaya ya Ikungi kuwasaka na kuwakamata wavamizi wa msitu wa
Minyughe wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo Makazi, kilimo na
Ufugaji kinyume na Tangazo la serikali (GN) ya kuanzisha hifadhi ya
msitu wa Minyughe ya Mwaka 2007.
Katika
Oparesheni hiyo Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mambo mengine pia
iliyobaini ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa
Vijiji na Vitongoji ikiwemo kuwauzia mavamizi maeneo kwa kutoa Rushwa ya
fedha au Mifugo.
Mhe
Mtaturu ameiagiza Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU)
Kuwahoji wote wanaotuhumiwa katika sakata la kuruhusu wavamizi wa
hifadhi ya msitu.
Alisema
kuwa Ni aibu kubwa kwa viongozi kujihusisha na tuhuma mbalimbali
zinazoichafua serikali, Kuvunja heshima na Uaminifu wa wananchi kwa
serikali yao.
"Dhambi
ya viongozi kuwaacha kwa makusudi wananchi waharibu misitu itaendelea
kuwatafuna viongozi hao kwani wamewasababishia wananchi kuingia hasara
ya kuchomewa nyumba zao ambazo walidhani Ni makazi ya kudumu, Ni dhahiri
kuwa hatuwezi kuvumilia Nchi ikawa inaongozwa ovyo ovyo ilihali Kuna
sheria, taratibu na kanuni" Alikaririwa Mhe Mtaturu
Mhe
Mtaturu pia alisema kuwa ili kunusuru misitu kuharibiwa na wavamizi
itaundwa Bodi ya Misitu ambayo itashirikisha Wajumbe kutoka kila Kijiji
katika Vijiji 24 vlivyopo katika Kata 8 zilizopitiwa na msitu huo wa
hifadhi.
Pia
aliwataka viongozi wa Vijiji, Kata na Kamati zote za misitu
kushirikiana kwa karibu na serikali ili kutunza misiti kwani ndio Msingi
wa uimarishaji wa Mazingira na uoto wa asili.
Mhe
Mtaturu alisema kuwa dhamira ya kuhifadhi misitu Ni kutunza Mazingira
na uoto wa asili hivyo wananchi kufanya shughuli za kibinadamu Ni
kinyume na sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002.
Sambamba
na hayo pia Mhe Mtaturu aliwasihi wananchi kuanza kuandaa mashamba
kwani msimu wa Kilimo umekaribia huku akiwasisitiza kuendelea kumuunga
Mkono Rais wa Awamu ya Tano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kazi kubwa ya kusimamia
Rasilimali za Nchi anayoifanya.
Mhe
Mtaturu alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa
jengo litakalotumika kwa ajili ya kituo cha polisi cha muda huku
Akielekeza wananchi, serikali ya kijiji na Kata kusaidia ukarabati wa
kituo hicho sambamba na ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Kata ya
Makilawa.
Hifadhi
ya msitu wa Minyughe ilianzishwa kwa Tangazo la serikali (GN) Mwaka
2007 ina jumla ya hekta 264,600 ina manufaa makubwa katika utunzaji wa
mazingira na uoto wa asili kwa urahisi wa upatikanaji wa mvua na urahisi
katika uimarishaji wa sekta ya kilimo sambamba na ushoroba (Njia ya
Tembo).
Mwenyekiti
wa Kijiji Cha Mtavira aliyejiuzuru Ndg Jilala Lutelemula akizungumza
mbele ya wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara kabla ya kujiuzuru.
Mkazi
wa Kijiji cha Mtavira Wilayani Ikungi Ndg Nchambi Kadawi akieleza
changamoto inayowakabili wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UONGOZI NA WANANCHI MWINGINE AJIUZULU MBELE YA DC MTATURU
Reviewed by crispaseve
on
03:10
Rating:
Post a Comment