SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI
SERIKALI
imewataka wananchi kuunga mkono juhudi za usafi kwa kunawa mikono na
sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu ili kujenga Taifa
lenye watu wenye afya bora.
Akizungumza
katika kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni
iliyofanyika Kata ya Kiwalani, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Ubora wa Mamlaka ya Majisafi na
Majitaka Dar es Salaam(DAWASA), Dk Sufiani Masasi alisema kama Taifa ni
muhimu kuwekeza nguvu katika kuelimisha jamii hasa umuhimu wa kunawa
mikono na majisafi na sabuni ili kujenga Taifa lenye afya bora.
Akizungumza
na jumuiya ya wananchi, waalimu na wanafunzi wa shule za msingi Umoja,
Yombo, Mwale na Bwawani, Dk Masasi alisema DAWASA ni mdau muhimu wa
usafi wa mazingira ndio sababu waliamua kuadhimisha wiki hiyo kwa kutoa
elimu kwa walimu 44 kutoka katika shule hizo pamoja na baadhi ya
viongozi wa serikali ya mtaa ili wawe mabalozi
wazuri katika kuwaelimisha wanafunzi juu ya umuhimu wake.
Alisema
kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Mikono safi kwa manufaa ya
sasa na baadae’ inaikumbusha jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono na
sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu.
Hivyo
alitaka juhudi za pamoja zichukuliwe kuhakikisha wanafunzi wanaelewa
umuhimu wa kunawa mikono kwani wao ndio wazazi wa siku zijazo na kwamba
DAWASA itaendelea kuunga mkono kampeni za usafi hasa kwa kuendelea
kubuni na kutengeneza miundombinu ya majisafi katika Maeneo mbalimbali
ya jiji.
Dk
Masasi alisema tayari DAWASA imefanikiwa kufikisha mradi huo wa majisafi
kwa shule hizo ambapo utanufaisha wanafunzi 5123 pamoja na zahanati ya
eneo hilo na kwamba itaendelea kufadhili miradi ya aina hii ili kuunga
mkono juhudi hizo za usafi wa mazingira.
Mkufunzi
wa mafunzo kwa walimu wa shule hizo, Juhudi Nyambuka ambaye ni Afisa
Afya Manispaa ya Temeke alipongeza juhudi za DAWASA katika kusaidia
jamii kupata huduma za majisafi na kueleza zitasaidia kupunguza magonjwa
yanayosababishwa na ukosefu wa maji.
Katika
maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma rasmi za maji ya bomba DAWASA,
jumuiya za wananchi pamoja na wadau wa maendeleo wamekuwa wakijenga
miradi ya maji kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira kwa
jamii.
Miradi hiyo ipo katika maeneo mbalimbali kama vile Ukonga, Yombo, Kitunda, Mbagala, Kijichi, Feri,Kigamboni.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Wanafunzi
wa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Kiwalani wakishiriki igizo lenye
lengo la kuelimisha jamii umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni
wakati wa kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni
yaliyofanyika Kiwalani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI
Reviewed by crispaseve
on
04:41
Rating:
Post a Comment