WAKAZI WA WILAYA YA SAME WAONGOZWA KUFANYA MAZOEZI NA DC SINYAMULE
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU
wa Wilaya ya ISame Mkoa wa Kilimanjaro, Rosemary Sinyamule ameongoza
mazoezi ya wakazi wa Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya utamaduni
waliojiwekea watumishi na wakazi wa eneo hilo kila ifikapo mwisho wa
wiki.
Dc
Sinyamule amesesma kuwa mazoezi yamekuwa ni utamaduni hivyo wananchi
hao upata fursa ya kujumuika na viongozi wao katika siku ambazo sio za
kazi na kuweza kupata nafasi ya kuzungumza mambo ya kawaida yanayohusu
maisha yao ya kila siku katika mfumo wa kawaida .
"
leo wananchi wamepata fursa muhimu ya kusikiliza maelekezo ya afya
kutoka na umuhimu wa mazoezi kutoka Kwa mganga Mkuu wa Wilaya ya Same .
Dr. Andrew ambaye aliwataka wakazi wa eneo hilo kutunza afya kwa
kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki hili kuweza kujiepusha na magonjwa
yasiyokuwa ya lazima" amesema Dc Sinyamule.
DC
Sinyamule ameongeza kuwa katika kuadhimisha wiki ya kumbukumbu ya Baba
wa Taifa Hayat Mwl Julius Nyerere ni kila mmoja kuona namna
anavyomuenzi kwani alikuwa Mazalendo na alipigania Uhuru akiwa katika
umri mdogo hivyo kuwasisitiza Vijana kufanya yale yote yaliyofanywa na
Mwalimu katika harakati zake.
DC
Sinyamule alimaliza kwa kuwashukuru wananchi wa Same Kwa kuendelea
kujitokeza Kwa wingi. Pia aliwakumbusha kila mmoja kujipangia ratiba ya
mazoezi kila siku. na si kungoja siku moja Kwa mwezi.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja na Wanachi waliojitokeza katika Mazoezi Wilaya ya Same.
Wakazi wa Wilaya ya Same wakiwa katika Mazoezi ya Pamoja yaliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Rosemary Sinyamule.
WAKAZI WA WILAYA YA SAME WAONGOZWA KUFANYA MAZOEZI NA DC SINYAMULE
Reviewed by crispaseve
on
08:03
Rating:
Post a Comment