SERA YA VIWANDA HAITAFANIKIWA IWAPO HATUTAENDANA NA MABADILIKO MAKUBWA YA SOKO LA WAKULIMA
Wananchi
pamoja na wanachama wa CUF wa Kijiji cha Ughandi wakimsubiri kwa hamu
Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Prof.Ibrahimu Lipumba kumsikiliza
sera za chama na kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Delphina
Mngazija.
Mwenyekiti
wa CUF Taifa, Prof.Ibrahimu Lipumba (wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na
Mkurugenzi wa wanawake wa chama hicho, Salama Masudi kwenye viwanja vya
mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida
Vijijini kabla ya kuongea na wananchi hao.(Picha zote Na Jumbe
Ismailly).
Na,Jumbe Ismailly, SINGIDA
MKURUGENZI
wa wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Salama Masudi amesema
kuwa sera ya viwanda nchini haiwezi kufanikiwa iwapo hatutaendana na
mabadiliko makubwa ya soko la wakulima na ikiwezekana katika mpango
mzima wa mapinduzi ya kilimo wenye lengo la kuwawezesha wakulima wa
chini kuelekea soko kuu la dunia kuweza kuinua kipato kutoka kwa
wananchi maskini kabisa.
Mkurugenzi
huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa kumnadi
mgombea ubunge wa chama hicho kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi
mdogo wa jimbo la Singida Kaskazini uliofanyika katika Kijiji cha
Ughandi, wilaya ya Singida vijijini.
Alifafanua
Salama kwamba baada ya wakulima kuwa wamewezeshwa hususani katika
maeneo hayo wanayotoka ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo,basi
kuwezeshwa kwa viwanda hivyo kunawezekana kabisa kutoka maeneo muhimu
kulingana na mazao yanayotokana na uwezeshwaji wa viwanda hivyo.
Hata
hivyo Salama alisisitiza pia kwamba katika miaka yote wananchi wa jimbo
hilo wamekuwa wakipelekewa wagombea wanaume ambao wameshindwa kukidhi
haja zao kwa kuwa wanaguswa na matatizo yanayowashika wanawake
wenyewe,lakini mwaka huu CUF imewaletea mwanamama huyo mahiri na ambaye
wanaamini ndiye suluhisho pekee la matatizo ya wananwake.
“Tunaomba
kwa namna ya pekee na utulivu mkubwa tunaomba kura kwa akina mama
mtusaidie kuweza kumsaidia mama Delphina Mngazija kwa kuwa ninyi ndio
wengi kabisa katika upigaji wa kura na mnatumiwa kuwa chambo cha
kuwakandamiza wananchi”alisisitiza Salama.
“Tumewaletea
mama huyo anaguswa na changamoto zinazotukbili sisi wanawake,wengi wetu
hapa tunaumizwa na sera mbovu,tumekuja na kampeni pekee kupitia
mgombea wa chama chetu ‘Mwanamke tua ndoo maana yake akiwa sauti ya
Bunge kupitia Singida kaskazini anaweza kuongea na serikali kupitia
mifuko ya jimbo ili aweze kuleta visima vitakavyosaidia akina mama
kupunguza adha ya maji katika maeneo mnayoishi”alifafanua
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo wa wanawake Taifa alionyesha pia kukerwa na
baadhi ya watu au vyama vinavyosusia chaguzi,na kwamba vitendo vya aina
hiyo ni kinyume na demokrasia pamoja na upatikanaji wa maendeleo ya
nchi.
Hivyo
Salama alitumia wasaa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wa jimbo la
Singida kaskazini kutosusia chaguzi kwani kwa kufanya hivyo wanapoteza
haki zao za msingi za kikatiba.
“Niwaombe
wananchi wa kata hii,hususani katika kata hii ya Ughandi hususani wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM) mtupigie kura chama cha wananchi CUF,siyo
dhambi kabisa iwapo wananchi wenyewe kwa mapenzi mliyonayo mmemchagua
mtu ambaye ni chaguo lenu na anayewahurumia,lakini badala yake ameletwa
mtu kupitia kwenye njia zisizoeleweka”alibainisha Mkurugenzi.
Hata
hivyo mkurugenzi huyo alitumia mkutano huo kuwashawishi wananchi wa
kata ya Ughandi kutokichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kile
alichokiita ni nyimbo zilizokosa utekelezaji wake.
Akizungumzia
CUF kiongozi huyo wa chama alibainisha kuwa katika kipindi cha
takribani miaka ishirini tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikitetea
maslahi ya watanzania wote na kutoa mfano kwamba chama hicho
kinachoongozwa na Prof.Ibrahimu Lipumba amekuwa akiandaa mijadala mbali
mbali iliyochangia kuleta maendeleo.
Naye
mgombea ubunge wa jimbo la Singida kaskazini kupitia Chama Cha
Wananchi (CUF),Delphine Mngazija akiomba kura kwa wananchi wa Kijiji
cha Ughandi aliahidi kwamba endapo watampa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao
ataenda Bungeni kutetea akina mama waondokane na adha ya kutembea na
mabeseni,ndoo pamoja na mipira ya kujifungulia.
Alifafanua
mgombea huyo kwamba maana mama mjamzito akishakuwa na ujauzito hupatwa
na mawazo ya kuondoka kwenda kujifungua kwa kuanza kufikiria ni namna
gani atakavyonunua ndoo,beseni na mipira.
“Ninawaomba
ridhaa yenu akina mama mambo ya kwenda hospitali na kwenda kubeba
mabeseni niende kuwatetea nipigane na hilo kwa akina mama kwa sababu
taasisi ya afya ina mambo mengi kwani mama akijifungulia nyumbani
akimchukua mtoto wake kumpeleka hospitali hatapokelewa”alisisitiza
mgombea huyo.
SERA YA VIWANDA HAITAFANIKIWA IWAPO HATUTAENDANA NA MABADILIKO MAKUBWA YA SOKO LA WAKULIMA
Reviewed by crispaseve
on
09:13
Rating:
Post a Comment