UVCCM KIBAHA MJINI YAWATAKA VIJANA KUSIMAMIA KWA VITENDO MAPINDUZI
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.
JUMUIYA
ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjini Kibaha mkoani Pwani
imesema Taifa linawategemea vijana katika dhana nzima itakayothibitisha
wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yanayolikabili
Taifa hili.
Aidha
imekemea tabia ya kujigawa na kuweka makundi baina yao kwani kwa
kufanya hivyo ni kudidimiza harakati na juhudi za kuimarisha jumuiya na
kupambana kimaendeleo .
Mwenyekiti
wa UVCCM Mji wa Kibaha, Azilongwa Bohari aliyasema hayo, mara baada ya
jumuiya hiyo kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi
pamoja na kuchangia damu units 22 hospitalini hapo katika kuadhimisha
miaka 54 ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hata hivyo ,alisisitiza umoja na mshikamano kwa kundi la vijana.
Azilongwa
alisema, serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile
ya Mapinduzi ya Zanzibar ,zinatakiwa kuona vijana wake wanachemchem ya
maendeleo badala ya kuwa dimbwi la matatizo mitaani.
Aliwaasa vijana kwa umoja wao kujishughulisha na kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kujiinua kimaisha .
"Tukielekea
kwenye uchumi wa kati kuna kila sababu ya kupambana na umasikini,tukiwa
kama vijana ,tuondokane kuwa matatizo kwenye jamii bali tuwe wapiganaji
katika maendeleo na maisha yetu " alisema.
Pamoja
na hayo ,Azilongwa aliwaomba wanachama na viongozi wa jumuiya hiyo
kuanzia ngazi ya chini kushikamana ili kujidhatiti kwa lengo la kujenga
ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020.
Aliwataka
viongozi wa chama na jumuiya kuendelea kuongeza wanachama wapya ambao
ndio mtaji kwao na wapiga kura halali kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Azilongwa
hakusita kusisitiza vikao vya mara kwa mara na kuwataka viongozi wa
UVCCM wilayani hapo kushiriki katika vikao muhimu ili kujadili na kubuni
njia mbadala za kuongeza wanachama na kuinua maendeleo ya jumuiya.
Akielezea
zoezi la kuchangia damu, alishukuru wanachama waliojitokeza kuchangia
na kuwezesha units 22 ambazo kwa hakika zitasaidia kuongeza mahitaji
yanayotakiwa.
Alisema
wamelenga kuchangia damu hospitalini hapo, kutokana na mahitaji makubwa
na hospitali hiyo kupokea majeruhi wa ajali nyingi zinazotokea mara kwa
mara kwenye barabara kuu ya Morogoro.
Nae
katibu wa mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini,Method Mselewa,alisema mbali
ya hayo wanatembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mkuza na kutoa
misaada iliyotokana na ushirikiano wao na hisani kutoka kwa mbunge wa
jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na mkewe Selina Koka.
Mselewa alimshukuru mbunge huyo na familia yake kwa ushirikiano wao .
Baadhi
ya viongozi na wanachama wa jumuiya ya vijana ya Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) Kibaha Mjini, Pwani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kufanya usafi ,na kujitolea kuchangia damu units 22, katika hospitali ya
rufaa ya mkoa ya Tumbi ikiwa ni sehemu yao ya kuadhimisha miaka 54 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.(picha na Mwamvua Mwinyi).
UVCCM KIBAHA MJINI YAWATAKA VIJANA KUSIMAMIA KWA VITENDO MAPINDUZI
Reviewed by crispaseve
on
09:12
Rating:
Post a Comment