MWANRI AAGIZA WATOTO WASIPORIPOTI SHULE WAZAZI WAO WAKAMATWE
SERIKALI
Mkoani Tabora imeagiza kukamatwa mara moja wazazi au walezi ambao hadi
kufikia Jumatatu ijayo (15, January 2018) watakuwa wameshindwa
kuhakikisha kuwa watoto wao waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza
mwaka huu watakuwa hajaripoti katika Shule walizopangiwa.
Agizo
hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afisa Elimu Mkoa iliyoakuwa
ikionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na
Kidato cha kwanza mwaka 2018 bado wengi wao hawajaripoti katika Shule
walizopangiwa.
Alisema
kuwa kufikia Jumatatu ijayo anataka kupata taarifa na majina ya
wanafunzi wote waliochangiwa ambao hawako shuleni ikiwa na majina ya
wazazi wao ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa kwa kosa
la kumkoshesha watoto haki ya kupata elimu.
Mwanri
aliongeza kuwa viongozi wa kuanzia mitaa, vitongoji, vijiji , Kata na
Wilaya ni vema wahakikishe wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa ambao
hawako shuleni ili kujua walipo na wanafanya nini kwa kuwa inawezekana
wapo ambao tayari wameshaozeshwa.
Alisisitiza
kuwa wakikuta mtoto yupo nyumbani na mzazi wake hataki kumpeleka Shule
wamukamate mzazi wake ili hawawezi kuwajibika kwa uzembe wake.
“Hapa
tutakwenda kwa Sera ya mbanano…kama kiongozi lazima umbane mzazi ambaye
hadi hivi sasa hajampeleka mtoto shule wakati wenzake wameshaanza
masomo na ikibidi mfikisheni katika vyombo vya Sheria ili ajibu
mashitaka yake ya kunyima mtoto haki yake ya elima”alisema Mkuu huyo wa
Mkoa wa Tabora
Akitoa
taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati wa ziara ya kukagua zoezi la
upandaji miti kwa ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari ,Katibu Tawala
Msaidizi (Elimu) Suzan Nussu alisema kuwa hali ya watoto kuripoti katika
Shule za Sekondari kwa wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Kidato cha
Kwanza mwaka huu bado sio nzuri kwa baadhi yao hawajafika shuleni hadi
hivi sasa.
Alisema
kuwa katika Shule ya Sekondari ya Ngulu iliyopo Sikonge walichaguliwa
watoto 130 lakini hadi hivi sasa wamejiunga 44, Shule ya Sekondari
Usisya iliyopo Urambo wamechaguliwa 130 lakini waliripoti ni 54 na Shule
ya Sekondari Nanga Sekondari iliyopo Igunga waliochaguliwa ni 160
lakini walioripoti ni 7 hadi kufikia sasa.
Nussu
alisema kuwa kuchelewa kuripoti kwa wanafunzi hao sio tu kunarudisha
nyuma maendeleo ya watoto hao kwa sababu ya kuachwa na wenzao bali pia
kunasababisha usumbufu kwa walimu kuanza upya kuwafundisha wanafunzi
waliochelewa ili waweze kwenda na kasi ya wenzao.
Alitoa
wito kwa wazazi kuhakikisha ifikapo mapema wiki ijayo watoto wote wawe
wamefika Shule kwani tayari Serikali ilishafuta ada na hivyo hakuna
kisingizio ambacho kinaweza kumsababisha mtoto kushindwa kuanza masomo
yake kwa ajili ya faida yake na Taifa kwa ujumla.
Nussu
alisema kuwa michango mingine inapangwa na wazazi wa watoto wa Shule
husika kwa kukubaliana na Kamati za Shule na hivyo hakiwezi kuwa kikwazo
kwa watoto kushindwa kuhudhuria masomo yao.
Kwa
upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ngulu Israel Mwambikwa alisema
kuwa amekuwa akipata tatizo kutoka kwa baadhi ya wazazi kushindwa kutoa
hata michango waliokubaliana katika vikao vyao ya kutoa kilo 10 za
mahindi ,kilo mbili za maharage na shilingi 17,000/- ambazo wazazi
walikubaliana kama mahitaji ya chakula cha kila mtoto kwa mwezi.
MWANRI AAGIZA WATOTO WASIPORIPOTI SHULE WAZAZI WAO WAKAMATWE
Reviewed by crispaseve
on
09:11
Rating:
Post a Comment