MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza
na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya ziara ya kikazi
katika Hospitali hiyo na Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili
kubaini changamoto zilizopo za upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na
kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar
es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza,
Chrispin Kayola.
Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya
pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao mazungumzo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya
pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea wateja wa
MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni pamoja na
Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo katika
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.
Katika
ziara hiyo iliyofanyika jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu
amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na
kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30
Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi
maalumu.
Bwanakunu
alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo
katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.
Akizungumza
akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema anazitambua
changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na wamedata msaada
wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara
nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.
Kuhusu
vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba
kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila
hospitali kuleta kwa wakati wake.
"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa " alisema Bwanakunu.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni asilimia 80 .
"Changamoto
iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya macho na meno
ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji tuliyonayo,"
alisema.
Kwa
upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala,
Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na
MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by crispaseve
on
14:56
Rating:
Post a Comment