Header AD

JK afungua shule Sekondari Mlimani-Matemwe, Unguja

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia vitabu vya masomo katika maktaba ya shule mpya ya Sekondari ya Mlimani Matemwe muda mfupi baada ya kuifungua rasmi jana.Kulia ni Ofisa mwandamizi kutoka ofisi ya Benki ya Dunia nchini anayeshughulikia masuala ya elimu Bwana Nobuyuki Tanaka na kushoto ni Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Mohamed Mzee Choum.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi(kulia) na Afisa mwandamizi  kutoka katika kitengo cha elimu katika ofisi ya Benki ya Dunia nchini Bwana Nobuyuki Tanaka wakikata utepe wakati wa hafla ya ufunguzi wa Shule ya Sekondari ya Mlimani  Matemwe huko Zanzibar jana.Shule hiyo imejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Mainduzi Zanzibar na Benki ya Dunia. Picha na Freddy Maro wa Ikulu
Reviewed by crispaseve on 05:10 Rating: 5

No comments

Post AD