Header AD

RAIS KIKWETE ASHIRIKI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIGURUNYEMBE. MOROGORO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013  akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea
 Rais Jakaya Mrisho  Kikwete akiwasili akimkabidhi mjumuisho wa michango Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude  katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe  iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013 
Rais Jakaya Mrisho  Kikwete akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni   Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kwa watawa  keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja. Aliitoa keki hiyo kama zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa na watawa hao
 Rais Jakaya Mrisho  Kikwete na  Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude  katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na kamati ya harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa  harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
 Sehemu ya waliohudhuria  harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Picha na Ikulu
Reviewed by crispaseve on 10:35 Rating: 5

No comments

Post AD