UN TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA MAENDELEO DUNIANI 2013 IKIONYESHA NCHI ZINAZOENDELEA 40 ZIMEPIGA HATUA KUBWA SANA YA MAENDELEO YA BINADAMU
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba
ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 – Kuchomoza kwa
Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa
mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri
na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti
iliyopita. Hata
hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa
ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima
ujumla wa maendeleo katika Jamii. Bw.
Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa
hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia
vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda
lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.
Picha
Juu na chini ni Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwapokea wageni
mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wanafunzi wa vyuo
vikuu, Maprofesa, na wadau wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi
waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 uliofanyika
jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.
Mratibu
Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi
wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa
Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema
sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya
kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka
kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela. Lakini
pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa
mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na
kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya
kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha. Aidha
amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga
mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za
kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu
nyingine duniani.
Post a Comment