Ziara ya rais Kikwete Makete mkoa wa Njombe..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete mwishoni mwa juma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa shati lililotengenezwa na
wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete baada
ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa juma.
Rais akitoka kuweka jiwe la msingi madarasa ya kidato cha tano shule ya sekondari lupalilo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi Sarah
Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji pamoja na
mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili October 28, 2009 baada
ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha Lupalilo
wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV na
kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake wote
kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga
akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha
yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongeana wananchi wa kijiji cha Ivalalila
wilayani Makete baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha afya cha
kijiji hicho mwishonimwa juma.Picha na IKULU.
Reviewed by crispaseve
on
07:16
Rating:
Post a Comment