BAADHI YA MATUKIO 10 AMBAYO YALITIKISA NCHI YA TANZANIA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013
IMEANDIKWA NA JOSEPHAT LUKAZA KWA MSAADA WA MTANDAO
Ikiwa imebaki siku Moja Kumaliza mwaka 2013, Mwaka ambao umekuwa na matukio mengi tu kama miaka mingine iliyopita lakini Pia Mwaka huu una mtukio Mengi tofauti na Miaka iliyokwisha Pita. Na yafuatayo ni baadhi ya Matukio 10 ambayo yaliweza kuitikisa nchi na Kuchuku Nafasi katika Kurasa mbalimbali za Magazeti, Mitandao ya Kijamii na hata Kwenye TV.
Ikiwa imebaki siku Moja Kumaliza mwaka 2013, Mwaka ambao umekuwa na matukio mengi tu kama miaka mingine iliyopita lakini Pia Mwaka huu una mtukio Mengi tofauti na Miaka iliyokwisha Pita. Na yafuatayo ni baadhi ya Matukio 10 ambayo yaliweza kuitikisa nchi na Kuchuku Nafasi katika Kurasa mbalimbali za Magazeti, Mitandao ya Kijamii na hata Kwenye TV.
1:UKUSANYAJI WA MAONI YA KATIBA MPYA
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Makunduchi Aziza Mcha, akikabidhi barua yake yenye maoni yake kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa kutoa maoni ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, wakati tume hiyo ilipofika katika Wilaya ya Kusini Unguja kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
Katika Kipindi cha Mwezi wa 6 kuelekea Mwezi wa 7 mwaka 2013 Tume ya Mabadiliko ya katika Ilikua inapita katika maeneo mbalimbali kwaaajili ya Kukusanya maoni ya wananchi kwaajili ya uundwaji wa Katiba Mpya Ya Tanzania. Hii ni moja ya Tukio Kubwa sana lililotokea Katika Kipindi cha Mwaka 2013.
2: MABILIONI YA USWISI
.jpg)
Katika Kipindi hiki cha Mwaka 2013 Kuliibuka Sakata la Vigogo wa Nchi Kuhifadhi pesa zao katika Mabenki ya Uswisi, Sakata hili liliibuliwa bungeni Na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya Chadema Mh Zitto Z Kabwe na Ndio Utata ulipokuwa mkubwa na hatimaye Benki Kuu ya Uswisi ikatoa ripoti juu ya Nchi ambazo raia wake wahifadhi pesa katika Benki zilizopo Nchini Humo. Katika Hali ya Kushangaza Tanzania ni Moja ya Nchi za Kiafrika ambayo inaongoza kwenye list ambayo Raia wake wanaongoza kuhifandhi jumla ya Kiasi cha Dola Milioni 196 ambazo sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 313.6. Hili nalo ni tukio mojawapo lililotikisa Nchi kwa Mwaka 2013.
3: MACHAVUKO KUHUSU GESI HUKO MTWARA

Baada ya Kugundulika kwa Gesi asilia yenye Thamani ya Dola Za Kimarekani Bilioni 500 mwanzoni mwa mwaka wa 2012 bila shaka Kukatokea sakata la mvutano wa gesi kati ya Serikali na Wakazi wa Mji wa Mtwara kuhusiana na Kutoka Kwa Gesi hiyo kuelekea Jijini Dar Es Salaam. Mnamo Mwishoni mwa Mwezi wa Disemba Mwaka 2012 tulishuhudia vurugu kubwa ambazo zilipelekea Kuchomwa kwa Nyumba za watu Huko Mtwara kutokana na Vurugu za Kugombania gesi na Hatimaye Vurugu hizo zikaendelea kuchukua hatamu hadi kuingia mwaka 2013 ambapo pia vurugu na mvutano wa gesi itoke au isitoke uliendelea kutawala katika vichwa vya wakazi wa Tanzania kuhusiana na Gesi asilia hiyo iliyogundulika huko Mtwara hii ni Moja pia ya Tukio lililotikisa Nchini Mwaka 2012 hadi mwanzoni mwa Mwaka 2013.
4: MILIPUKO YA MABOMU ARUSHA: WAKATI WA UZINDUZI WA KANISA LA ST JOSEPH ENEO LA OLESITI NA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA
Shambulizi katika kanisa Katoliki la Arusha la sababisha taharuki.
Mnamo tarehe 5 Mei 2013 Katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo eneo la Olasiti Jijini Arusha Lilikumbwa na Dhoruba ya Kulipuliwa na Bomu la Kurushwa Kwa Mkono wakati wa Uzinduzi wa Kanisa hilo ambapo Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mwakilishi wa Papa Kutoka Vatican. Tukio hilo lilipelekea Watu wawili Kupoteza maisha Na Wengine zaidi ya Kumi ambao walifikishwa katika Hospitali ya Meru Mkoani Arusha..Tukio Hili ni Moja ya Tukio la Kulipuliwa kwa Bomu katika Kipindi Cha Mwaka 2013. Vilevile Ndani ya Miezi miwili katika Mwaka 2013 kulitokea mlipuko wa bomu wakati wa Chama Cha Siasa cha Chadema kilipokuwa kikifanya Mkutano wao na kupelekea Majeruhi na baadhi kupoteza maisha.
5: KUWASILI KWA RAISI WA MAREKANI MH BARACK OBAMA NCHINI TANZANIA.
Mnamo Mwezi wa 7 tarehe 1 na 2 Raisi wa Marekani Mh Barack Obama kwa mara ya kwanza aliwasili nchini Tanzania na Kupokelewa na Mwenyeji wake Raisi Kikwete akiwa katika Ziara yake Ya kutembelea Nchini Za Afrika Ambapo Tanzania Ni Moja ya Nchi alizotembelea Mh Obama. Katika Ujio Huu Hali ya Hewa Nchini Tanzania Hususani katika Jiji la Dar Ilikuwa Tofauti Kidogo kutoka na Mambo mengi kubadilika kutoka Na Ulinzi mkali ambao ulikuwepo katika Kipindi cha Siku Chache kabla ya Kuwasili Raisi Huyo wa Marekani Ambapo baadhi ya Barabara zilifungwa kwaajili ya Kutumiwa na Raisi Huyo na Kupelekea Baadhi ya Sehemu kuwa safi
6: ASKARI SABA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA WAFARIKI DUNIA HUKO DARFUR SUDAN BAADA YA KUSHAMBULIWA
Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
Mnamo tarehe 13 Julai 2013 Askari wetu 7 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walipoteza maisha kutokana na shambulizi la ghafla huko Darfur Nchini Sudan wakati wakitekeleza Wajibu wao Wa kulinda amani katika Jimbo Hilo. Hilo ni moja la Tukio Kubwa kabisa ambalo Limeitika Nchi yetu ya Tanzania kutokana na Kupoteza rasilimali watu na mashujaa wetu hao ambao walikuwa katika Wajibu wao wa kulinda Amani Huko Darfur Sudan
7: OPERESHENI KIMBUNGA
Askari wa jeshi la polisi Afande Mwijage akitoa somo la Uraia kwa watoto waliyokuja kuiangalia helikopta kijiji cha Benako wakati wa Doria ya kusaka wahamiaji haramu na mifugo yao katika pori la Kimisi Wilayani Ngara , ikiwa ni mwendelezo wa awamu ya pili ya Opereshani Kimbunga ambayo imeshaanza .
Hili ni tukio la Kihistoria ambalo limetokea nchin Tanzania ndani ya Mwaka 2013 ambappo operesheni kimbunga ililenga kuwaondoa wahamiaji wote haramu ambalo walikua wakiishi kinyume na Sheria na taratibu katika Nchi Ya Tanzania. Hili ni tukio nalo Ambalo lilichukua Kurasa Katika Vyombo Mbalimbali vya Habari nchini Tanzania
8: KUMWAGIA TINDIKALI ZANZIBAR
Katika Kipindi cha Mwaka 2013 matukio ya Umwagiaji wa Tindikali kwa baadhi ya watu yaliweza Kulipotiwa huku akiwemo Padri Joseph Monesmo na Baadhi ya Raia Wa Kigeni Huko Zanzibar. Matukio haya yalianza kutokea Kwa MAra ya Kwanza Baada ya Kumwagiwa Tindikali Mwandishi wa Habari Saed Kubenea mnamo mwaka 2008.Huu Ulikuwa kama mwendelezo katika Mwaka 2013 ambapo Watu kadhaa walilipotiliwa kumwagiwa tindikali Huko Zanzibar akiwemo Padri Joseph na Raia wawili wa Kigeni.
9: SHEKHE PONDA AITIKISA NCHINI

Sheikhe Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza wakati akielekea katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kusikiliza kesi yake inayomkabili. Picha na Juma Mtanda
Mwaka huu ulikuwa mwaka wa Matukio Tanzania Ambapo kwa Mara Nyingine tena Shekhe Ponda aliendelea Kuitikisa Nchi, Haitosaulika kuwa Ponda aliweza kutengeneza stori Katika Vichwa Vya Habari katika Vyombo Mbalimbali vya Habari Nchini
10: MAPIGANO NDANI YA UKUMBI WA BUNGE
Kwa Mara ya Kwanza Katika Historia ya Siasa za Tanzania Ni mwaka 2013 ndio umeingia katika Vitabu vya HIstoria Nchini Kwa Kutokea vurugu Kubwa ndani ya Jumba la Watunga Sheria aka Bunge ambapo Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aliweza kuzua Kizaizai katika Ukumbi Huo wa Bunge na Kupelekea Askari wa Bunge Kutumia Nguvu kwaajili ya Kumtoa Nje ya Ukumbi wa Bunge ambap hali nayo haikuwa shwari kwani askari mmoja wa Bunge alilipotiwa kujeruhiwa na Mbunge wa Mbeya Mjni Mh Joseph Mbilinyi. Hili ni Tukio Moja Kubwa sana katika Medani za Siasa hapa Tanzania tokea kuanzishwa Kwa Vyama vya Upinzani.
BAADHI YA MATUKIO 10 AMBAYO YALITIKISA NCHI YA TANZANIA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013
Reviewed by crispaseve
on
12:42
Rating:



Post a Comment