Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi chapata viongozi wapya,Steve Nyerere aibuka Mwenyekiti.

Pichani
ni Uongozi wa juu wa Chama cha Wasanii wa Filamu hapa nchini.a.k.a
Bongo Muvi,kulia ni Katibu Mkuu,William Mtitu,Mwenyekiti,Steven Mengere
a.k.a Steve Nyerere,Katibu Msaidizi Bi.Devotha Mbaga,Mweka hazina Mkuu,
Issa Mussa Cloud pamoja na Makamu Mwenyekiti ,Mahsein Awadh maarufu kama
Dk Cheni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa hapo
jana na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo waliokutana kwenye viwanja vya
Lidaz club,jijini Dar.
Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa Uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii
wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo
wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili,
Diamond peke yake anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu,Dk Cheni akiwashukuru wadau
mbalimbali waliotoa ushirikiano mkubwa kwa namna moja ama nyingine
kuhakikisha uchaguzi wa viongozi katika tasnia hiyo wanapatikana,ikiwa
ni shemu ya kuhakikisha maendeleo yanazidi kupatikana ndani ya chama
hicho
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi,William Mtitu
akizungumza machache na kuwashukuru Wanachama na wadau mbalimbali katika
suala zima la kufanikisha kuwachagua viongozi wawatakao,ambao
watahakikisha chama chao kinasimama imara.

Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu nchini a.k.a Bongo
Muvi,Vincent Kigosi a.k.a Ray akitoa shukurani kwa wanachama na wadau wa
tasnia yao waliofika kwenye uchaguzi huo,Ray amewataka viongozi hao
wapya kuendelea kuijenga tasnia hiyo katika suala zima la kuhakikisha
inaendelea kukua siku hadi siku.
Ray akifafanua jambo kwa ufasaha mara baada ya kukabidhi nafasi yake ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya Steve Nyerere. PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.
Chama cha Wasanii wa Filamu a.k.a Bongo Muvi chapata viongozi wapya,Steve Nyerere aibuka Mwenyekiti.
Reviewed by crispaseve
on
11:29
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
11:29
Rating:





Post a Comment