Uganda yaunda kikosi maalum
Wanajeshi wa Uganda
Jeshi la Uganda, limeweka vituo
vya kukabiliana na majanga na dharura, ili kuharakisisha shughuli ya
kuwatuma wanajeshi wake haraka endapo kutatokea dharura au mzozo katika
kanda ya Afrika Mashariki.
Wanajeshi wa Uganda, wamekuwa wakiwasaidia
wanajeshi wa Sudan Kusini kupambana na wapiganaji wa waasi, kwa muda wa
mwezi mmoja uliopita.
Mwandishi
wa BBC mjini Kampala anasema amesema kuwa huenda serikali ya nchi hiyo
inataka kushirikishwa katika majukumu kama hayo siku zijazo.
Wanajeshi wa Uganda vile vil vile wanatunza amani nchini Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Wanajeshi hao pia wamewahi kuhudumu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.
Muungano wa Afrika umekuwa na mpango wa kuunda
kikosi maalum cha kukabiliana na majanga na mizozo, lakini pendekezo
hilo halijaidhinishwa na vingozi wa serikali za nchini wanachama wa
muungano huo wa AU.
Uganda yaunda kikosi maalum
Reviewed by crispaseve
on
12:30
Rating:

Post a Comment