RICK ROSS ANUNUA JUMBA LA KIFAHARI LA BONDIA WA ZAMANI EVANDER HOLLYFIELD.
C.E.O wa Crew ya M-M-M-M-Maybach Music(Double M), Rapa Rick
Ross ameripotiwa kununua jumba kubwa la kifahari ambalo kipindi cha
nyuma lilikuwa linamilikiwa na mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani,
Evander Hollyfield.
Jumba hilo lililopo katika mji wa Georgia Marekani, ukubwa
wake ni mita za mraba 54,000 lenye jumla ya vyumba 109, Bwawa kubwa la
kuogelea na eneo la wazi lenye ukubwa wa eka 235, kwa taarifa ni kwamba
jumba hilo linagharimu kiasi cha dola milioni 1 kuweza kulihudumia kwa
muda wa mwaka mzima. Mpaka sasa Rapa huyo ameshalipia kiasi cha dola za
kimarekani Milioni 8…Tazama picha hapa chini.
Wadau wanaofuatilia gemu ya muziki wamedai kwamba Rozzay
amefanya matusi hayo ikiwa ni kama kumlipizia Rapa 50 Cent ambaye
aliwahi kununua jumba la kifahari lililokuwa na eka 50,000 kutoka kwa
bondia Mike Tyson kwa gharama ya Dola za kimarekani Milioni 4.1 kutokana
na wawili hao kuwepo katika bifu, ivyo mkae tayari usishangae kusikia
Rick Ross Kamng’ata sikio 50 Cent.
RICK ROSS ANUNUA JUMBA LA KIFAHARI LA BONDIA WA ZAMANI EVANDER HOLLYFIELD.
Reviewed by crispaseve
on
05:54
Rating:

Post a Comment