MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI NA ZINAZOISHI MAZINGIRA HATARISHI UNAORATIBIWA NA TASAF YAIMARISHA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI
Afisa
Habari wa TASAF (mwenye T-SHIRT NYEUPE) Estom Sanga akizungumza na
mmoja wa wanafunzi ambao kaya yake inanufaika na mpango wa kunusuru kaya
masikini.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo ambao kaya zao zimo kwenye
mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani Bunda mkoani Mara.
Samweli
George na Anna George ambao wanatoka katika kaya inayonufaika na mpango
wa kunusuru kaya masikini wakiwa makini kuelekea shuleni.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo ambao kaya zao zimo kwenye
mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani Bunda mkoani Mara.
Habari kutoka Bunda mkoani Mara kutoka kwa Estom Sanga wa TASAF.
Michuzi tafadhali nisaidie tutawasiliana baadaye kidogo..
Mpango
wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umewezesha
mahudhurio ya wanafunzi katika shule za msingi kuimarisha kwa kati ya
asilimi 80 hadi 100.
Wakizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea baadhi ya shule ambako wanafunzi
wanaotoka katika kaya masikini ambazo ziko katika mpango huo ,wamesema
mahudhurio ya wanafunzi kwa sasa ni mazuri hali iliyochangiwa kwa
kiwango kikubwa na uboreshwaji wa huduma wanazopata baada ya kaya zao
kuingizwa katika mpango wa kunusuru kaya masikini.
Hivi
sasa wanafunzi ambao walikuwa wakikosa masomo kwa kukosa vifaa vikiwemo
sare,madaftari,kalamu na hata viatu kwa sasa wanahudhuria masomo yao
bila matatizo na hata uelewa wao umeelezwa kuongezeka tofauti na kabla
ya mpango huo kuanza.
Miongoni
mwa masharti ambayo kaya masikini zilizoingizwa kwenye mpango wa
kuzinusuru ambao unaratibiwa na TASAF ni kuhakikisha kuwa watoto wa kaya
husika wanahudhuria shuleni na hata kupata huduma za lishe na matibabu
pale wanapoyahitaji.
MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI NA ZINAZOISHI MAZINGIRA HATARISHI UNAORATIBIWA NA TASAF YAIMARISHA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI
Reviewed by crispaseve
on
02:56
Rating:

Post a Comment