WAANDISHI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI KWENYE KURIPOTI BUNGE LA KATIBA
Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan akifungua
warsha ya siku moja kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya nafasi
ya watetezi wa Haki za Binadamu katika Katiba mpya.
.waambiwa waache kamari ya majongoo kuhusu serikali mbili ama tatu
.watetezi wa haki za binadamu, waandishi watoswa kwenye rasimu ya Katiba
Na Damas Makangale, Dodoma, MOblog
WAANDISHI
na Wahariri wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa kuzingatia maadili
ya uandishi wa habari na kuweka mbele maslahi ya taifa wakati wa
kuripoti Bunge maalum la katiba. MOblog inaripoti.
Akifungua
warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya watetezi
wa haki za binadamu na asasi za kirai katika katiba mpya jijini Dodoma,
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan
amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya
haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa kuzingatia weledi wa fani yao
na maadili ya uandishi.
“waandishi
wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa kuweka mbele maslahi ya
taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta suluhu, amani, mshikamano
na utulivu,” amesema.
Mratibu
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Ndg. Onesmo
Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la wabunge wa katiba
na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa haki za binadamu
katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku moja
uliofanyika mjini Dodoma.
Amesema
waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao wanaweza kushauri na
kushirikiana na serikali na mamlaka zingine kupatikana kwa katiba mpya
yenye tunu za taifa, Sululu aliongeza kwa kuweka
hoja zao kwa ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta mshikamano na
ushirikiano wa kitaifa katika kudumisha amani na haki za binadamu
nchini. Amesema kwamba kupitia bunge la katiba
wanahabari ni kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi na
kuelimisha umma jinsi sheria na haki za binadamu zinavyoweza kulinda na
katiba ya nchi.
Mwezeshaji, Mwandishi wa Habari, Mwanasheria, msomi na mjumbe wa Bunge la Katiba Ali Uki akizungumza kwenye warsha hiyo.
“waandishi
kwa kutumia nafasi yao wanaweza kushauri kwa kurekebishwa baadhi ya
sheria, vifungu ili kuweza kulinda haki za binadamu nchini kwa kupitia
bunge maalum la katiba,” aliongeza. Alisisitiza
Mhe Sululu kwamba bunge la katiba halijadili kuhusu ama serikali mbili
au tatu kwa sababu kuna mambo mengi kwenye rasimu ya katiba
yakujadiliwa.
“kwa
jinsi mnavyoripoti kuhusu serikali mbili ama tatu ni kama mchezo wa
kamari ya majongoo jamani katiba siyo muungano tu,” amesema. Kwa
upande, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC),
Onesmo olengurumwa amesema ingawaje kwenye rasimu ya katiba hawajatambua
watetezi wa haki za binadamu bali wataendelea kushauriana na wajumbe
kupata mwafaka wa jambo hilo.
Meza kuu, Ndg. Onesmo Olengurumwa akiwa na Mgeni rasmi Samia Suluhu Hassani kwenye warsha hiyo.
“Rasimu
ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya mashirika yasiyo ya
kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama zilivyoanishwa
kikatiba,” amesema
Olengurumwa
aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia haijatambua wasaidizi wa kisheria
wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa msaada mkubwa kisheria kwenye
ngazi za vijijini. Amesema
ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua mjadala wa katiba ili
misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya utetezi wa haki za
binadamu nchini.
Olengurumwa
amesema waandishi wa habari kama vile watetezi wa haki za binadamu
maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na katiba ya nchi ili kujenga
mazingira mazuri ya haki za binadamu nchini. Hivi
karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa Serikali
tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
na Serikali ya Tanganyika. Mjadala
wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya
Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma.
wahadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally
wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na
Channel Ten hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Nyamsenda
amesema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume hiyo, ambayo
haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu rasimu ambayo
haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya wananchi na
maoni yao.
WAANDISHI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI KWENYE KURIPOTI BUNGE LA KATIBA
Reviewed by crispaseve
on
21:57
Rating:
Post a Comment