Header AD

PIGO : GURUMO AFARIKI DUNIA HOSPITALI YA MUHIMBILI.


Gurumo
Marehemu Maalim Muhidin Gurumo enzi za uhai wake.
Wapenzi wa muziki wa dansi wamepatwa na Pigo kubwa kufuatia kifo cha mwanamuziki mkongwe   ‘Maalim Muhidin  Gurumo’ kilichotokea mchana wa leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliyokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba Mzee Gurumo alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Awali Gurumo aliwahi kuwa kiongozi wa bendi kongwe nchini ya Msondo Ngoma ambayo alipata kuiongoza kwa kipindi kirefu kabla ya kuamua kustaafu muziki. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tabata Makuburi.
Blogu ya Larrybway91 inawapa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
AMEEEEN!!!
PIGO : GURUMO AFARIKI DUNIA HOSPITALI YA MUHIMBILI. PIGO : GURUMO AFARIKI DUNIA HOSPITALI YA MUHIMBILI. Reviewed by crispaseve on 03:59 Rating: 5

No comments

Post AD