TAARIFA YA MELI YA MIZIGO ILIYOZAMA ZIWA VICTORIA

Watu 10 wamenusurika kufa maji katika ziwa
Victoria baada ya meli ya mizigo Fb Matara
kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari
tani 280 zilizonunuliwa katika kiwanda cha sukari
Kagera wakati ikitoka Bukoba kwenda jijini
Mwanza.
Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Mkombozi
fishing and marine transport limited, imezama
ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani
280, mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza
aitw ye V.h.Shah, ambapo mkurugenzi wa
kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza
kwamba meli hiyo imezama ikiwa katikati ya visiwa
vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku
na kuongeza kwamba hakuna mtu yeyote
aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo.
ITV imeshuhudia meli hiyo ikiwa imepinduka huku juhudi za wafanyakazi wa kampuni hiyo kuipundua
zikiwa zinaendelea bila mafanikio, huku baadhi yamashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hiyo kuzama ni kutokana na dhoruba kali
ambapo wametoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini kuzingatia utabiri unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kuepusha
maafa.
Meli hii inayoonekana pichani ni mfano wa meli iliyozama,ambayo ilianza safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na kapteni Erick Lasan mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu
Sumatra kanda ya ziwa, umethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 280 za mizigo na abiria 100.
Chanzo ITV
TAARIFA YA MELI YA MIZIGO ILIYOZAMA ZIWA VICTORIA
Reviewed by crispaseve
on
05:41
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
05:41
Rating:

Post a Comment