KAMPUNI YA MAFUTA NA GESI YA SWALA (TANZANIA) PLC INATANGAZA UZINDUZI WA IPO.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya
Swala (Tanzania) PLC, David Mestres Ridge (kulia), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu ufunguzi wa ofa ya awali kwa
umma ijulikanayo kwa kifupi (IPO) ambayo itakuwa na hisa za kawaida,9,600,000.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ARCH Financial $ Investment Adivisory
Limited,Iyen Nsemwa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) PLC, Abdullah Mwinyi
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, kuhusu ufunguzi wa ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kwa kifupi (IPO)
ambayo itakuwa na hisa za kawaida,9,600,000. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Swala, David Mestres Ridge na Mkurugenzi Mkuu wa ARCH Financial $ Investment
Adivisory Limited,Iyen Nsemwa.
===== ======= =========
Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) Plc leo
imetangaza ufunguzi wa ofa yake ya awali kwa umma ijulikanavyo kwa kifupi kama
("IPO") yenye hisa za kawaida 9,600,000. Kampuni itakuwa ikiuza kila
hisa kwa bei ya shilingi za Kitanzania
500 kuanzia tarehe 9 juni 2014 mpaka tarehe 4 Julai 2014.
Tangazo hili limekuja
wiki moja baada ya kampuni kupokea
idhini yake rasmi kutoka Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania
("CMSA"), na kuifanya kuwa ni ofa ya kwanza kufanyika kwenye sekta ya
mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Swala
Bwana David Mestres Ridge alisema, "Tunafuraha kuwa, leo Kampuni ya mafuta
na gesi ya Swala (Tanzania) Plc imezindua rasmi mpango wake wa ofa ya awali kwa
umma ijulikanayo kama IPO. Hii ni hatua kubwa si tu kwa ajili ya Swala lakini
pia kwa Tanzania na watu wake kwa ujumla. . Kuwekeza hisa katika mafuta na gesi
ni moja ya njia za kupanua wigo wa kiuchumi kwa mtu yeyote na inaruhusu mtu
yeyote kumiliki hisa katika biashara hii inayokua kwa kasi ".
Bwana Ridge alizidi kusema,
"Tunaishukuru sana Serikali ya Tanzania, Shirika la mafuta na gesi
Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kwa kuturuhusu
kuwa kampuni ya kwanza ya Mafuta na gesi katika Afrika Mashariki inayomilikiwa
na umma. Kwa niaba ya wakurugenzi wote wa Swala napenda kuukaribisha rasmi umma
kuwekeza katika Kampuni ya mafuta na
gesi ya Swala (Tanzania) Plc ".
Mhe.
Abdullah Mwinyi, ambaye ni Mkurugenzi wa Swala Tanzania Plc aliongeza,
"Kumekuwa na mjadala mkubwa kwa wazawa katika sekta hii ya uchimbaji wa
mafuta na gesi; Tumefurahia kwamba leo kampuni ya mafuta na gesi ya Swala imekuwa
ya kwanza kuanza utekelezaji wa haja za wazawa katika sekta hii ya mafuta na
gesi. Tunaamini kwa dhati kabisa kwamba Watanzania wapewe nafasi ya kushiriki
katika biashara ya mafuta na gesi; ufunguzi huu wa IPO unaruhusu wao kufanya
hivyo."
Fomu za maombi na nakala ya
Waraka wa matarajio zitakuwa zinapatikana katika ofisi zote za Mawakala wenye
leseni kutoka soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE) walioko karibu yako, matawi
ya Benki ya CRDB Plc na ofisi za Arch Financial & Investment Advisory Ltd.
Ofa iko wazi kuanzia tarehe 9 Juni 2014 mpaka 4 Julai 2014.
Kwa sasa hakuna
ukomo wa kiwango cha juu cha hisa, lakini kiwango cha chini cha kununua ni hisa
100 kwa mtu. Waraka wa Matarajio wa kielektronikia unapatikana kwenye tovuti ya
kampuni www.swala-energy.co.tz au www.nihisa.com.
KAMPUNI YA MAFUTA NA GESI YA SWALA (TANZANIA) PLC INATANGAZA UZINDUZI WA IPO.
Reviewed by crispaseve
on
14:00
Rating:
Post a Comment