CFAO YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WAMILIKI WA MALORI YA MERCEDES BENZ NCHINI
Msimamizi wa ufundi wa Magari aina ya Mercedes Benz kutoka kampuni ya CFAO Motors Bw. Winner Mushi (wa tatu kushoto) akionyesha matumizi ya kifaa maalum cha ukaguzi wa Malori ya Mercedes Benz (Star Diagnosis Machine) kwa baadhi ya mafundi na wasimamizi wa ufundi wa magari ya kampuni ya Bakhresa Group.
Bakhresa Group ni mmoja wapo wa wateja wa CFAO Motors ambao wanamiliki malori ya Mercedes Benz. Bw. Heico Herzog Mtaalamu wa ufundi (Flying Doctor) kutoka Mercedes Benz Ujerumani,(wa tatu kulia) akisimamia shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bw. Mushi.
Wengine ni Key Account Manager wa Mercedes Benz, Bw. George Washington (kulia), Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif (kushoto), Jarangi Nyabagara ambaye ni fundi wa Mercedes Benz (wa pili kushoto), na aliyechuchumaa ni Mohammed Shariff Meneja wa Karakana ya Bakhresa Group.
Na Mwandishi Wetu,
KAMPUNI ya CFAO Motor Tanzania hivi karibuni imezindua huduma mpya ya “Service Camp” ambapo chini ya huduma hii wa wamiliki wa malori yanayotengenezwa na Mercedez Benz watapata huduma ya ukaguzi bure na mafunzo kwa madereva wao.
Akizungumza na mwandishi wetu, jijini Dar es Salaam Key Account Manager wa Mercedez Benz, Bw George Washington amesema kwamba wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuweza kuwahudumia wamilimi wa magari hayo kwa karibu zaidi.“Mpango huu utapeleka huduma karibu na wateja na kwa kuwa hapo mwanzo wamiliki wa malori walikuwa hawapati huduma za matengenezo vizuri barani Afrika,” amesema.
Amesema kuwa kuna upungufu katika kuwahudumia wamiliki wa malori ya Mercedez Benz Afrika na hivyo wameona ni busara kuja na ‘Service Camp’ ili kuwapeleka wateja huduma za matengenezo na mafunzo kwa madereva wao huko walipo. Aliongeza kwamba huduma hiyo ya ‘Service Camp’ itakuwa ikitolewa kwa njia mbili tofauti ambazo ni kwenda kwa mteja na kukagua malori bila gharama yoyote.Amesema kwamba vile vile chini ya huduma hiyo watakuwa wakitoa mafunzo kwa madereva wa malori ili waweze kujajua vizuri magari hayo pindi wanapopata tatizo la kiufundi.
Bw.Washighton aliongeza kwamba vile vile watakuwa wanawafundisha madereva jinsi vipuri vya Mercedez Benz vinavyopaswa kuwa ili kuweza kutambua vipuri bandia kwenye soko la nchini au karakana mbalimbali. “Tunawaonesha vipuri halisi na vipuri bandia kwa sababu kuna madhara katika kutumia vipuri bandia ambapo madhara yanaweza yasionekane katika muda wa siku chache bali huonekana baada ya muda mrefu,”
“Ukianza kuangalia gharama ya kutengeneza gari baada ya madhara kutokea unakuta gharama yake ni kubwa kuliko ambapo ungetumia vipuri halisi,” alieleza Bw Washington.
Alisisitiza kwamba kwamba hatua ya pili ni kuweka kambi barabarani ambapo malori mengi ya Mercedes Benz yanapita, hivyo kila ambaye anamiliki lori aina ya Mercedes Benz na anataka kufanyiwa ukaguzi, hupata huduma hiyo bila gharama, na hatimaye taarifa kamili zake za ukaguzi kurudishwa kwa mmiliki wake.
Washington amesema kwamba kampuni ya CFAO inataka kuwa karibu zaidi na wateja wake, kwani inataka wateja waone kwamba kuna watu wanaowajali ili kudumisha na kuimarisha uhusiano kati yao na wateja wao.
CFAO YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WAMILIKI WA MALORI YA MERCEDES BENZ NCHINI
Reviewed by crispaseve
on
14:02
Rating:
Post a Comment