Picha na Taarifa Rasmi Kutoka Wizara ya Fedha:Serikali imepokea Shilingi Bilioni Moja (1,275,000.00)Kutoka TIPER ikiwa ni Gawio Ambalo Kampuni Hiyo imekuwa ikilipa Kwa Wanahisa Wake Kila Mwaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile (wa pili
kushoto) akipokea hundi yyenye thamani y ash. Bilioni moja ktoka TIPER
gawio la hisa katika hafla iliyofanyika ljana mjini Dodoma. Wa kwanza
kshoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair, Wa pili kulia ni
Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim
Mruma na Wizara ya fedha Kaimu Msajili wa Hazina Elius Mwakabinga (wa
kwanza kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair (kushoto) akitoa
taarifa ya kampuni ya TIPER invyoshikiana na Serikali katika kukuza
uchumi na kuongeza soko la ajira nchini wakati wa kukabidhi gawio
linalotolewa na kampuni yake kwa serikali jana mjini Dodoma. Kulia ni
Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim
Mruma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servarcius Likwelile (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji
wa TIPER Daniel Belair (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kupokea gawio
la hisa za Serikali katika hafla iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Wanafuata ni baadhi wa Maafisa waandamizi wa Wizara Fedha.Picha na habari na Ingiahed Mduma na Eleuteri Mangi-Wizara ya Fedha
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA
Serikali imepokea shilingi
bilioni moja kutoka TIPER ikiwa ni gawio ambalo kampuni hiyo imekuwa
ikilipa kwa Wanahisa wake kila mwaka.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile alipokuwa akipokea gawio
hilo katika hafla iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Dkt. Likwelile alisema kuwa gawio
hilo litaelekezwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2013/2014
unaomalizika kwa kuangalia maeneo ambayo yanawagusa wananchi ikiwemo
sekta ya elimu, afya na maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo, Daniel Belair alisema kuwa si mara ya kwanza
kwa kampuni yake kutoa gawio kama hilo kwa Serikali ambapo mwaka jana
muda kama huu kampuni ilitoa kiasi kama hicho kama gawio Mkurugenzi huyo alisema kuwa
kampuni yake imeendelea kufanya vizuri katika kukuza maisha ya kijamii
na kiuchumi ambapo kwa sasa inafanyakazi kwa saa 24 na siku saba za
wiki.
Kwa kuzingatia utendaji huo,
kampuni ya TIPER imekuwa kichocheo kukuu cha kuzalisha ajira nchini
ambapo hadi sasa asilimia 99 ya wafanyakazi wake ni nguvu kazi ya
Watanzania.
Naye Mwenyekiti
Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma alisema
kuwa imekuwa ni muhimu kwa kampuni yao kuwa na akiba ya kutosha ya
mafuta kwa nchi na kuleta mafanikio makubwa ya upatikanaji wa mafuta
nchini.
Aidha, TIPER Prof. Mruma alisema
kuwa kwa sasa kampuni yao imejikita katika kuleta mafuta yaliyosafishwa
nchini ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.
“Kwa sasa tunaleta mafuta
yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi ambayo yanazalisha tope jingi
ambalo limekuwa ni hatari katika kutunza mazingira yetu” alisema Prof.
Mruma
Pamoja na ufanisi huo, kumekuwepo
na changamoto za kuboresha mkataba wa utendaji na usimamizi wa hesabu
masuala ambayo wanahisa wote wawili wanaendelea kuyafanyia kazi kwa
madhumuni ya kuwa na matokeo mazuri zaidi kwa pande zote.
Kiutendaji kampuni ya TIPER
inaendeshwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania ambayo inahisa zenye
asilimia 50 na Kampuni ya Oryx Energies SA asilimia 50.
Pamoja na
Tanzania Kampuni ya Oryx Energies SA inafanyakazi katika mnchi
mbalimbali duniani ambazo ni Benin, Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Guinea
Conakry, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Afrika
Kusini, Uhispania (Visiwa vya Canary), Togo, Uganda na Zambia.
Imetolewa na :
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Dodoma
13/6/2014
Picha na Taarifa Rasmi Kutoka Wizara ya Fedha:Serikali imepokea Shilingi Bilioni Moja (1,275,000.00)Kutoka TIPER ikiwa ni Gawio Ambalo Kampuni Hiyo imekuwa ikilipa Kwa Wanahisa Wake Kila Mwaka.
Reviewed by crispaseve
on
13:43
Rating:
Post a Comment