Tahadhari ya Picha:Msaada wa Kijana Mwanaid Saleh
Mama Mzazi wa Kijina Mwanaidi Bi Jina akimpatia uji mtoto wake wakiwa
katika wodi ya hospitali ya mnazi mmoja wakiendelea na Tiba baada ya
kuhamishiwa hapo kutoka hospitali ya jeshi bububu, ili kuendelea na
huduma hiyo ya matibabu wakisubiri kupata michango ili kuweza
kumsafirisha nje ya nchi kupata matibabu zaidi.
---
Maendeleo ya michango wa Kumchangia Kijana Mwanaid Saleh Kupata Matibabu.
Tunashukuru kwa Michango Yenu
kwani Kijana Mwanaid Saleh, tayari amehamishiwa Hospitali Kuu ya rufaa
Mnazi Mmoja kutokea Bububu akiendelea na Matibabu kusubiri hatua zaidi
za Matibabu Nje ya Nchi
Tunawashukuru wananchi wliojitokeza kumchangia Mwanaid Saleh,ili kupata Matibabu Kwa sasa Michango imefikia shilingi 444, 000/= Ikiwa katika Benki ya PBZ Tawi la Malindi Zanzibarhadi sasa.
Wananchi waliojitokeza kumchangia kupitia Tigo Pesa 0715 424152.
Omar Shamte Shs.4,000/= ,
Kupitia Wakala wa Tigo Pesa Shs 10,000/=, Ziada Kikunga Shs 6000/=
Khamis Suleiman M-PESA Shs 48,000/= na Maryam Hilal Shs. 3000/=
Bado michango yenu inahitajika
na tutazidi kukupeni taarifa kadri tutakavyoipokea kwani jumla ya pesa
zinazohitajika takriban milioni 15 ili zimwezeshe kufanyiwa matibabu.
Tahadhari ya Picha:Msaada wa Kijana Mwanaid Saleh
Reviewed by crispaseve
on
13:45
Rating:
Post a Comment