YOUNG JEEZY MIKONONI MWA POLISI KWA KUKUTWA NA BUNDUKI
Rapa mzaliwa wa Atlanta nchini Marekani, Jay Jankins AKA
Young Jeezy amekamatwa na polisi kwa madai ya kukutwa na bunduki baada
ya mtu mmoja kufariki Dunia kwa kupigwa risasi kwenye Tamasha la muziki
la Wiz Khalifa lililofanyika Mountain View mjini California.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 22 ambapo mtu huyo
aliyetambulika kwa jina la Eric Johnson mwenye miaka 38 alifyetuliwa
risasi tatu mfululizo akiwa backstage na baadae kufariki Dunia
hospitalini.
Inaelezwa kwamba jumapili iliyopita(Agosti24) polisi
walifanikiwa kukuta bunduki aina ya Rifle ikiwa ndani ya basi la Young
Jeezy waliyoamini kuwa ni yake na hivyo kuwalazimu kuwatia nguvuni
wapambe wake pia.
Kwa mujibu wa mtandao wa E! Online umeripoti kwamba watu
wengine waliokamatwa ni pamoja na Kena Marshall, Peter Maynard, David
Kuniansky-Altman, William Gilmore, na Alexa Beason huku dhamana ya Jeezy
ikiwa dola za kimarekani milioni moja.
YOUNG JEEZY MIKONONI MWA POLISI KWA KUKUTWA NA BUNDUKI
Reviewed by crispaseve
on
06:40
Rating:
Post a Comment