Header AD

JAJI : OSCAR PISTORIUS HAKUUA KWA KUKUSUDIA

Pistorius
Oscar Pistorius akiwa kizimbani
Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha wa mbio za Paralyimpiki, Oscar Pistorius amesema upande wa mashtaka umekosa kuthibitisha kikamilifu shtaka kuu la kwanza dhidi ya Pistoriuos kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuwia kutenda uhalifu huo alipomuua mpenzi wake River.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana katika siku ya wapendanao lakini amekana kumuua kwa makusudi na kusema alidhani mwizi amevamia nyumba.
Kwa upande wa mashtaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa makusudi baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana huku taarifa zaidi zikidai kuwa Jaji Thokozile Masipa huenda akachukua hadi Ijumaa yaani kesho kumaliza uamuzi wake.
Pistorius huenda huenda akafungwa jela miaka 25 kama atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
JAJI : OSCAR PISTORIUS HAKUUA KWA KUKUSUDIA JAJI : OSCAR PISTORIUS HAKUUA KWA KUKUSUDIA Reviewed by crispaseve on 01:19 Rating: 5

No comments

Post AD