Watanzania waaswa kutunza vipato vyao wawe na maisha bora.

Mwezeshaji
wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni jijini Dar es salaam
wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI
UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri
au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora
wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu. Katikati ni Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya na kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John
Masumba.

1 Mwezeshaji
wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (wa pili kulia) akimpongeza
Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Rose Mang’enya wakati wa
uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI” hivi
karibuni jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Taasisi
hiyo John Masumba na Afisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Eleuteri mangi
(kulia). (Picha na MAELEZO).
Taasisi
isiyo ya kiserikali ya MAYEPS Tanzania imezindua kitabu kiitwacho
“NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu
wanaofanyakazi ya kujiajiri au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi
ili waweze kuishi maisha bora wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya
kustaafu.
Akizungumza
na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es salaam, Meneja wa
Taasisi hiyo John Masumba amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wafanyakazi
katika jamii ya Kitanzania hawaweki akiba kwa ajili ya kuwekeza kwa
madhumuni ya kujenga uchumi.
Meneja
Masumba amesisitiza kuwa MAYEPS imetambua kwamba ikiandaa warsha moja
kwa mwezi juu wafanyakazi kufanya maamuzi yaliyo sahihi, itawafikia watu
600 kwa mwaka.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya aliwapitisha
waandishi wa habari juu ya yaliyomo kwenye kitabu hicho kwa kuendesha
warsha fupi iliyowafungua macho waandishi hao kuhusu namna ya kutunza
fedha kuandaa maisha ya baadaye.
Akinukuu
kauli ya mtaalamu wa uongozi John Maxwell Mwenyekiti huyo alisema kuwa
“Watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa hawatofautiani sana kiuwezo bali
wanatofautiana katika dhamira ya kufika kilele au upeo wa uwezo wao”. Mang’enya aliongeza kuwa jukumu la kujenga maisha binafsi lipo kwa muhusika binafsi, hivyo, watumishi wawe na msimamo sahihi utakaowawezesha kuwa na maisha bora.
Aidha, MAYEPS hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Umama na binafsi namna ya kupanga matumizi. Pia hutoa mafunzo ambayo
yatawezesha wafanyakazi kutambua kuwa fedha za mafao au pensheni
hupungua thamani mwaka hadi mwaka hivyo uwekezaji wa fedha hizo ni
muhimu ufanywe kwa uangalifu.
Watanzania waaswa kutunza vipato vyao wawe na maisha bora.
Reviewed by crispaseve
on
05:58
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
05:58
Rating:

Post a Comment