Header AD

YANGA YATWAA NGAO YA JAMII KWA KUITANDIKA BAO 3 – 0 AZAM FC

Yanga
Kikosi cha Yanga
Wakali ya Jangwani, kikosi cha Yanga kimefanikiwa kutwaa ngao ya jamii baada ya kuwapa kichapo cha magoli 3 – 0 wanalambalamba wa Azam Fc katika mchezo uliochezwa Jumapili ya Septemba 14 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil, Geilson Santos ”Jaja” aliweza kuipatia Yanga mabao mawili mnamo dakika ya 58′ na 66′   kabla ya Simon Mvuva  kukamilisha karamu hiyo ya magoli kwa kutupia bao la tatu mnamo dakika ya 88 na mchezo kumalizika kwa Yanga kutwaa Ngao ya Jamii.
Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Young Africans mbrazili Marcio Maximo alisema anawashukuru wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake hali iliyoplekea kucheza soka safi la kuburudisha linaloambatana na ushindi.
Aidha Maximo alisema baada ya ushindi wa leo maandaliz ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar yataanza siku ya jumanne ambapo kwa kesho ametoa mapumziko kwa wachezaji wote pamoja na benchi la Ufundi.
YANGA YATWAA NGAO YA JAMII KWA KUITANDIKA BAO 3 – 0 AZAM FC YANGA YATWAA NGAO YA JAMII KWA KUITANDIKA BAO 3 – 0 AZAM FC Reviewed by crispaseve on 03:55 Rating: 5

No comments

Post AD