BINGWA WA KUCHEZA NA PIKIPIKI ATUA NCHINI LEO KUWASHA MOTO COCO BEACH, DAR

MWANAMICHEZO
ambaye anacheza kwa kutumia pikipiki Bian Capper kutoka nchini Afrika
kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya
kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
Akizungumza
jana kabla kuonesha umahiri huo mchezaji wa pikipiki ambaye ni raia wa
Afrika Kusini anayefanya ziara katika nchi za Afrika kwa udhamini wa
kinywaji cha Redbull atakuwa nchini kwa ziara za ya maonesho ya kuonesha
namna ya kucheza na pikipiki kwa siku tatu.


Onyesho
la kwanza lilianza jana kwenye viwanja vya Coco beach , leo Jumapili
atakuwa Mlimani City na kesho Jumatatu atakuwa katika eneo la Ubungo
Tanesco ambako litakuwa onyesho lake la mwisho.
Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.


Wakati
huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club Blagina Mwihava
alisema kwamba wamemleta mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa
ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya
kucheza mchezo huo wenye mvuto.
“Hii
itakuwa ni shoo kwa watanzania ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu
wa aina yake .Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans
inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote ni ya wazi.
PICHA ZOTE NA VIDEO NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
BINGWA WA KUCHEZA NA PIKIPIKI ATUA NCHINI LEO KUWASHA MOTO COCO BEACH, DAR
Reviewed by crispaseve
on
05:32
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
05:32
Rating:

Post a Comment