Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ya TRA lafanyika leo jijini Dar

Mgeni
rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa
nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika leo Novemba
15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es
Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.

Kaimu
Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan
Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi
kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo
kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo
lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira
wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie
alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.



Sehemu
ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyakazi wa
NSSF ambao ni Waalikwa walioshiriki kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki
ya Mlipa Kodi wakifatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasmi,ambapo kauli
mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na
Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".

Mtanange
wa kukata na shoka kati ya Timu ya TRA na timu ya NSSF ulipigwa katika
Uwanja wa TCC Chang'ombe,Mtanange uliowatoa kifua Mbele vijana wa NSSF
kwa Mabao 4-2 dhidi ya wenzao wa TRA.

Mbio za kuku kwa kina Baba zilikuwa ni sehemu ya michezo iliyofanyika leo Uwanjani hapo.

Vijana
wa Kundi la Wanne Star wakionyesha makeke yao mbele ya wadau wa TRA
waliofurika kwa wingi kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar
es Salaam leo.
Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ya TRA lafanyika leo jijini Dar
Reviewed by crispaseve
on
06:16
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
06:16
Rating:

Post a Comment