MHE. MWAKYEMBE AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA TANZANIA, DUBAI, MHE. OMAR MJENGA

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harrisson Mwakyembe, amekutana na
kufanya mazungumzo ofisini kwake na Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa
Tanzania, Dubai.
Mhe. Mjenga amemueleza Mhe. Mwakyembe kuhusu mazungumzo
yake pamoja na Mhe. Gaith Alghaith, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege
la FlyDubai, kuhusu mpango wa shirika hilo kuingia makubaliano ya
ushirikiano pamoja na shirika la Ndege la Tanzania(Air Tanzania) ambako
Flydubai watatoa ndege tano zitakazochukua njia za ndani (domestic
routes) na zile za kikanda (regional routes).
Ushirikiano huu utasaidia kufufua njia zote za ATC na kuiwezesha ATC kuanza kupata mapato.
Njia za kikanda ni pamoja na Kinshasa, Lubumbashi, Goma,
Kigali, Bunjumbura, Entebe, Nairobi, Sychelles, Moroni, Madagascar,
Mauritius, Maputo, Lilongwe, Lusaka, Joharnessburg, na Harare.
MHE. MWAKYEMBE AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA TANZANIA, DUBAI, MHE. OMAR MJENGA
Reviewed by crispaseve
on
03:37
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
03:37
Rating:

Post a Comment