FID-Q AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAIFA LETU.
Mwanamuziki
wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda Fid Q akizungumza na waandishi
wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge wakati akitangaza kuanza
kwa kampeni maalum ya kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi
mbalimbali kwa njia ya matamasha inayoitwa(#Tuo8January). ambayo
itaanza jumamosi mkoani Njombe kutoka kulia ni Promota Tale Msanii
Dito na kutoka kushoto ni mtayarishaji wa muziki Lamar Fishcrabmusic na
Promota Said Fella wakiwa katika mkutano huo.
============= ======= ============
Msanii nguli wa miondoko ya
Hip-hop Fareed Kubanda – Fid Q amekutana na waandishi wa habari katika
ukumbi wa Sports Lounge katikakati ya jiji la Dar es Salaam, kujadili
maswala ya msingi yenye mustakabali chanya kwa maendelo ya taifa hili.
Ameitisha mkutano huu akiwa kama kijana na mwenye nafasi na ushawishi
kwa vijana wenzie katika ushiriki wa kuleta mabadiliko chanya na
maendeleo ya nchi yetu.
Fid Q amesukumwa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kutanabai kwamba vijana japo ni asilimia 80 ya taifa lakini hawana mwamko na msukumo wa kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi waowataka na wanaowaamini wanauwezo wa kuleta mabadiliko ya ki nidhamu kwenye masuala ya msingi ya taifa letu.
“Kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hasa hasa vijana wenzangu hawakifahamu, Nchi yetu ni changa sana. Vijana nchi hii chini ya umri wa miaka 35 ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu, wakati watu wazima zaidi ya miaka 60 ni asilimia chini ya 5 ya watanzania wote.
Hizi ni
takwimu za sensa iliyopita. Nimetanguliza takwimu mapema kwa sababu,
twakimu huwa hazisemi uwongo. Changamoto zinalolikumba taifa hili kwa
kiasi kikubwa zinatuathiri sisi vijana wa nchi hii ambao ndio wengi
wetu. Madhara yanayotokana na uongozi mbovu, vile vile yanatuathiri sana
sisi vijana kwa wingi wetu. Tutake tusitake, ustawi na kunawiri kwa
vijana ndio kutaamua mustakabali wa Tanzania, vijana tukilala basi na
Tanzania pia italala.” Alisema Fid Q.
FID-Q AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAIFA LETU.
Reviewed by crispaseve
on
04:56
Rating:

Post a Comment