WATANZANIA WASHEREHEKEA MIAKA 53 YA UHURU OAKLAND CALIFORNIA
Balozi
wa heshima Mhe. Ahmed Issa (watatu toka kushoto) akibadilishana mawili
matatu na mgeni rasmi wa sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara
Mhe. Dr. Saidi Mohamed Mtanda (wapili toka kushoto), mbunge wa Afrika
Mashariki na mwenyekiti kamati ya kudumu ya huduma za jamii katika Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Mtanda pia ni Mbunge wa jimbo
la Mchinga Mkoani Lindi. Kulia ni Cherry Mke wa Mhe. Ahmed Issa.

Balozi
wa Heshima Mhe. Ahmed Issa akitoa salamu za miaka 53 ya Uhuru na baadae
kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia wanaCalifornia katika sherehe za
miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyikia Oakland, California
siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014.

Mgeni
Rasmi Mhe. Dr. Saidi Mohamed Mtanda akihutubia Watanzania Oakland,
California siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014 katika sherehe za miaka 53
ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizosherehekewa na Watanzania na amarafiki
zao kwenye jimbo hilo la California.
Vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vikinogesha sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara California.
Watanzania
na marafiki zao wakifuatilia sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania
Bara iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014 Oakland, California
nchini Marekani.

Watatnzania wa California wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Dr. Saidi Mohamed Mtanda.
Kwa picha zaidi bofya HAPA
WATANZANIA WASHEREHEKEA MIAKA 53 YA UHURU OAKLAND CALIFORNIA
Reviewed by crispaseve
on
11:05
Rating:

Post a Comment