Header AD

AIBU KUBWA! MUUZA GENGE ACHEZEA KICHAPO KWA KUNASWA NA MKE WA MTU


Muuza genge aliyechezea kichapo baada ya kunaswa na mke wa mtu na kutembezwa mtupu mtaani.

Aibu kubwa! Muuza genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini hapa ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu Fumanizi hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha wanandoa hao.
Kikiwa kwenye mishe zake, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers mkoani hapa kilipenyezewa kuwepo kwa ‘uovu’ huo ambapo hakikulaza damu.

ENEO LA TUKIO OFM, ikiwa eneo la tukio ilijikusanyia madai mazito juu ya jamaa huyo kuwa amekuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake binafsi.
Ilidaiwa kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.

Baada ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa ‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa ‘ubuyu’ mume.
Ilisemekana kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.
Wananchi wakimshuhudia muuza genge huyo akihadhirika baada ya fumanizi.
Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa kulicheza ‘segere’.
LAIVU NA SUTI YA KUZALIWA
Mwenye mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana kama ilikuwa ‘tayari au bado’.
Akiwa na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu weweee...”

Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha.
Kwa upande wake, jamaa huyo aliyedaiwa kufumaniwa alipohojiwa na OFM, aligoma kuzungumza na badala yake alificha uso kwa aibu.
AIBU KUBWA! MUUZA GENGE ACHEZEA KICHAPO KWA KUNASWA NA MKE WA MTU AIBU KUBWA! MUUZA GENGE ACHEZEA KICHAPO KWA KUNASWA NA MKE WA MTU Reviewed by crispaseve on 21:42 Rating: 5

No comments

Post AD