Header AD

BAKI SALAMA KIMTANDAO UTUMIAPO SIMU ZA MKONONI


Watumiaji wa simu za mkononi wameendelea kukua  kadri siku zinavyo endelea na kumekua na maswali mengi jinsi gani mtu anaweza kubaki salama atumiapo simu za mkononi.
 
Hapa nitaangazia uhalifu mtandao unao ambatana na simu za mikononi na njia za matumizi salama ya simu za mkononi.Nianze kuangazia uhalifu unaoweza kusababishwa na simu za mkononi.
Swapping: Huu ni uhalifu mtandao unao kua kwa kasi hivi sasa maeneo mbali mbali unaotoa fursa kwa mhalifu mtandao kuwa na matumizi ya simu ya mtu bila ya mwenye simu kujua. Mara nyingi wahalifu mtandao wana lenga kuiba pesa au kuwasiliana na watu wa karibu wa mtumiaji halisi wa simu ya mkononi kwa sababu tofauti tofauti.

Hii inatokea pale mhalifu mtandao anapo kua amepata namba yako ya simu na kusoma  ratiba yako hasa muda gani unakua hauna matumizi makubwa na simu – Baada ya kujua hivyo kupitia programu zilizopo sasa zina mpa fursa kukutoa hewani na kuanza kuitumia namba yako ya simu  ambapo anaweza kufanya mengi baada ya kua na umilikihuo ikiwa ni pamoja na kutoa au kuhamisha pesa zako na pia kuitumia vibaya simu yako.

Shoulder surfing: Hii ni njia inayotumika na wahalifu mtandao kuweza kujua namba za siri anazotumia mmiliki wa simu kwa kuangalia pale mtumiaji wa simu anapofanya miama ya kifedha kupitia simu au kufungua simu yake.

Mhalifu baada ya kupata taarifa hizo anaweza kukwapua simu hiyo na kuitumia vibaya kwani tayari Alisha jua namba za siri unazotumia na pia kuweza kufanya miamala na simu hiyo. Inashauriwa kuwa makini sana uwekapo namba za siri kwenye simu yako kwa kuhakikisha hakuna anayeweza kutazama ufanyacho kupitia simu yako.
BAKI SALAMA KIMTANDAO UTUMIAPO SIMU ZA MKONONI   BAKI SALAMA KIMTANDAO UTUMIAPO SIMU ZA MKONONI Reviewed by crispaseve on 00:18 Rating: 5

No comments

Post AD