TIGER WOODS APOTEZA MENO YA BARAZANI
Mchezaji nyota wa mchezo wa gofu Duniani, Tiger Woods,
amejikuta akipoteza meno ya barazani wakati akimshuhudia mpenzi wake
Lindsay Vonn akitwaa taji la ubingwa wa Dunia wa mbio za kuteleza kwenye
barafu kwa mara ya 63 nchini Italia.
Ishu hiyo ilijiri baada ya Tiger Woods kum-sapraiz ‘Lindsey
Vonn’ ambaye alikuwa akishiriki katika fainali za michuano ya mbio
hizo za kuteleza nchini humo.
Wakala wa mchezaji huyo, Mark Steinberg, amenukuliwa akisema
kwamba Woods alipatwa na majanga ya kupoteza meno yake ya mbele wakati
wa purukushani na wandishi wa habari katika mbio hizo, ambapo mwandishi
mmoja wa habari aliyekuwa amebeba video camera alisukumwa na kujikuta
akimgonga mchezaji huyo eneo la mdomo.
Siku moja baada ya kutangazwa mshindi, Vonn aliandika ujumbe
mfupi kupitia ukurasa wake wa facebook akielezea kufurahishwa na ujio wa
kushtukiza wa mpenzi wake huyo katika fainali ya mchezo huo na
alishtushwa baada ya kuona hana meno ya meno.
”Pindi alipokuwa amesimama katika eneo la kumalizia mbio, kwa bahati mbaya paparazi alimgonga na kupoteza meno yake ya mbele”, aliandika Venno na kuongeza,”Hakulalamika au kuomba msaada maalum au usalama. Sisi sote wawili tulifurahia wakati wetu”
TIGER WOODS APOTEZA MENO YA BARAZANI
Reviewed by crispaseve
on
01:31
Rating:
Post a Comment