DWYANE WADE WA MIAMI HEAT APIGWA FAINI YA DOLA 15,000 NA NBA KWA KOSA HILI
Mchezaji
nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat, Dwyane Wade amejikuta
akipigwa faini ya dola za kimarekani 15,000 na shirkisho la mpira wa
kikapu NBA, baada ya kuonyesha ishara mbaya wakati wa mchezo baina yao
na Charlotte Hornets uliochezwa juzi Jumatano.
Rais wa shirikisho hilo, Rod Thorn alitangaza kumlima faini
mchezaji huyo usiku wa kuamkia leo, kwa kosa la kuonyeshea ishara ya
kidole cha kati mbele ya umati wa mashabiki uliokuwa ukitazama mchezo
huo.
Katika robo tatu ya mchezo huo, Wade anayechezea safu ya
ulinzi alionekana akitoa ishara hiyo licha ya tukio hilo kutokurushwa
hewani katika mchezo uliomalizika kwa Hornetts kushinda jumla ya vikapu
78 – 76 dhidi ya Heat kwenye uwanja wa Time Warner Cable.
DWYANE WADE WA MIAMI HEAT APIGWA FAINI YA DOLA 15,000 NA NBA KWA KOSA HILI
Reviewed by crispaseve
on
01:35
Rating:
Post a Comment