BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA UTUMIAJI WA SimBanking NA FAHARI HUDUMA WAKALA
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
BENKI
ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia
simu za mkononi ‘SimBanking’ kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama
‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni
kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa
kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.
Alisema
kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi
mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja
watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine
mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.
“Tunataka
kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni
sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,”.
Akielezea
namna ya kushiriki na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei
alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma
hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi
husika.
“Mshindi
ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi kwa kutumia SimBanking
au FahariHuduma katika mwezi husika, iwe ni kutumia fedha kwenda kwenye
akaunti nyingine, au kwenda kwenye mitandao ya simu au kulipia Ankara,”
alisema.
Kwa
upande wake ,Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari alisema
ubunifu ndio njia pekee itakayotatua changamoto, ni muda muafaka kwa
Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kujishindia zawadi.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’, kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam
BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA UTUMIAJI WA SimBanking NA FAHARI HUDUMA WAKALA
Reviewed by crispaseve
on
06:17
Rating:
Post a Comment