SIKU YA KIMATAIFA YA FARAGHA YA TAARIFA (DPD) NA YAKUZINGATIA
Mataifa
mbalimbali duniani ifikapo tarehe 28 ya kila mwezi wa kwanza wanaadhimisha siku
ya kimataifa ya faragha ya taarifa ambapo kunakua na matukio mbali mbali ya kuhamasisha
njia rafiki za kuweka salama taarifa za watu hasa wawapo mtandaoni. Taarifa
zaidi za siku hii "BONYEZA HAPA"
Siku
hii imekua ikitumika vizuri kwa ushirikiano mkubwa ma mashirika binafsi,
serikali na vyombo vya habari kukumbusha watumiaji mitandao kuzingatia matumizi
salama ya mitandao ili kubakisha taarifa za watumiaji mtandao salama.
Inafahamika,
ukuaji wa wa kasi wa Teknolojia umeambatana matumizi yasiokusudiwa wa
teknolojia ambapo umekua ukihatarisha sana ufaragha wa watumiaji wa teknolojia
hizo. Kwa kuzingatia hili siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa imekua
ikihimizwa kutumika vizuri kukumbusha watumiaji mtandao yale yanayoweza
kuhakikisha taarifa zao zinabaki salama watumiapo mitandao.
Kwa
uchache mambo kadhaa ya kuzingatia ili kuweza kulinda faragha yako ya taarifa ikiwa
ni ukumbusho ni kama yafuatayo:-
Kupitia
mahojiano maalumu katika kuadhimisha
siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa yaliyofanyika kati yangu na
kituo cha
radio cha East Africa pamepata kuanishwa kwa uchache mambo muhimu ya
kuzingatia
ili kuweza kujiweka salama utumiapo mtandao na kuhakiki taarifa zako
zinabaki
salama ambapo ni umakini wa kuperuzi tovuti pamoja na utumiaji wa
Hotspots (Wifi au Wireless) zinazotolewa bure katika maeneo ya
mkusanyiko.
Ufafanuzi
wa kujua jinsi gani utajua kama tovuti unayoitembelea ni salama au la – Kuna tool
maarufu ijulikanayo kama “WOT – Web Of Trust” ambayo inatoa msaada wa kutoa
tathmini ya tovuti. Inapo ona tovuti haiku salama inakutahadharisha unapojaribu
kuitembelea, ni vizuri ikatumiwa ili iweze kukupa msaada wa kujua kama
unachotembelea ni salama au la.
SIKU YA KIMATAIFA YA FARAGHA YA TAARIFA (DPD) NA YAKUZINGATIA
Reviewed by crispaseve
on
06:19
Rating:
Post a Comment