Dida Shaibu BlogBaada ya hivi karibuni kunukuliwa na gazeti moja la Udaku hapa Bongo akikiri kumaliza tofauti na aliyekuwa mume wake Ezdee na kudai kwa sasa wao ni marafiki wa kawaida na hawawezi kurudiana kutokana na kila mmoja kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Hatimaye mtangazaji wa kipindi cha mirindimo ya pwani kinachorushwa hewani na Times Fm, Dida Shaibu   ameamua kumuanika hadharani mpenzi wake  na kummwagia sifa kemkem ikiwemo ya kutompa stress na kuongeza kuwa hajawahi kupendwa namna hiyo.
Duu nilianza kulala ila nimeota ndoto mbaya wameniweka kwenye kinu wananitwanga, nimekurupuka, kwani saa ngapi? ahaaaaaa niko na shemeji yenu Saint Anne nashukuru ananipenda sana sijawahi kupendwa hivi anayesema mapenzi shubiri kuwa nae uyu noo stress…nitarudi kulala”, aliandika Dida kwenye ukurasa wake wa Instagram na ku-post picha ya mpenzi wake huyo hapo chini
Dida Shaibu Times
Huyu ndiye mpenzi mpya wa Dida Shaibu anayefahamika kwa jina la Saint Anna
Dida Shaibu
Dida Shaibu akimnadi mpenzi wake mtandaoni
Dida Shaibu Mchopanga
Dida Shaibu akiwa ameangusha kitandani kwake baada ya kutolewa stress na mpenzi wake Saint Anna