Mazishi ya mfalme wa Saudi Arabia
Viongozi wengi wa dunia wametuma risala za rambi rambi kwa utawala wa Saudia kufuatia kifo cha mfalme wao Abdullah.
Nchi kama vile Bahrain na Jordan zimetangaza siku arobaini za maombolezi kwa heshima yake.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon, amempongeza mflame huyo kwa juhudi zake za kutafuta amani katika mashariki ya kati.
Japo
mfalme Abdullah amesifiwa ndani ya nchi yake na hata baadhi nje ya
nchi, wanaharakati wa haki za binadamu wamejitokeza kukashifu utawala
wake wakisema kuwa alileta mabadiliko machache sana ya kusifika.
Saudi
Arabia ina ushawishi mkubwa katika mataifa ya Pakistan, Bangladesh na
India ambapo inafadhili miradi kadha na shule nyingi zinazotoa mafunzo
ya kidini.
Makundi nchini pakistan kwa muda mrefu yamekuwa
yakishutumu baadhi ya shule hizo ambazo yanasema zinaendesha kampeni za
chuki dhidi ya Washia
Chamgamoto inayomkabili mfalme huyo mpya ni
kuhakikisha kuwa msaada wa mamilioni ya ya dola hauwafikii wale
wanaounga mkono chuki.
Makundi ya haki za binadamu yanaamini kuwa
uongozi mpya wa saudi Arabia utatekeleza ahadi za muda mrefu za
kuboresha mazingira kwa mamilioni ya wafanyikazi wahamiaji kutoka nchi
za Asia.
Wanasema kuwa hadi sasa waajiri nchini Saudi Arabia wana usemi mkubwa juu wa wajiriwa wao.
:BBC
Mazishi ya mfalme wa Saudi Arabia
Reviewed by crispaseve
on
00:00
Rating:
Post a Comment