IKULU YA MAREKANI YAMSAKA ALIYEVUJISHA SELFIE YA MTOTO WA RAIS OBAMA MTANDAONI
Baada ya kuzagaa kwa habari juu ya kuvuja kwa picha aina ya
selfie kwenye mtandao wa Twitter kupitia akaunti ya Masked Gorilla
ambayo alipiga mtoto wa Rais wa Marekani, Barack Obama, Malia Obama
ikimuonyesha akiwa amevaa Tshirt ya Pro Era ambayo ni brand ya rapa
maarufu wa Brooklyn, Joey Bada$$ imepelekea ikulu ya Marekani kuanzisha
uchunguzi ili kuweza kubaini mtu aliyevujisha picha hiyo.

Malia Obama akiwa ametupia kitu cha Pro Era
Kwa mujibu wa Fox News imeripoti kwamba ikulu ya Marekani
inaangalia ni jinsi gani selfie hiyo ilivujishwa kwenye mtandao kwa mara
ya kwanza huku watu wakiwa hawana uhakika wa asilimia 100 kama picha
hiyo ni ya kweli.
Michelle Obama ameweka sheria kali kwa binti zake
kujihusisha na mitandao ya kijamii na huenda akawa hajapendezwa kabisa
na kitendo cha picha iyo ya binti yake kutumika kwenye blogu za Rap na
kupigia debe brand hiyo.
”Mimi bado si muhumini mkubwa wa Facebook kwa matumizi ya vijana wadogo”,
alisema Michelle wakati akihojiwa na mtangazaji Barbara Walters
akielezea jinsi alivyowadhibiti mabinti zake, Malia na Sasha kujihusisha
na mitandao ya kijamii.
IKULU YA MAREKANI YAMSAKA ALIYEVUJISHA SELFIE YA MTOTO WA RAIS OBAMA MTANDAONI
Reviewed by crispaseve
on
02:38
Rating:

Post a Comment