JERRY MURO AZUNGUMZIA MUSTAKHABALI WA KASEJA NA YANGA
Mkuu
wa Idara ya habari na mawasiliano ya Yanga Sc, Jerry Murro amezungumzia
kinagaubaga juu ya mustakhabali wa goli kipa Juma Kaseja baada ya
mashabiki na wapenzi wa soka kutaka kufahamu kinachoendelea kati yake na
uongozi wa timu hiyo.
Akichezesha taya na Clouds Tv michezo, Muro amesema kuwa
matatizo ya Kaseja na klabu ya Yanga yalianza kujionyesha baada ya yeye
mwenyewe kuona hapewi kipaumbele sana kwenye klabu iyo kutokana na
kukalishwa benchi tofauti na zamani alipokuwa akijulikana kama golikipa
nambari moja.
”Matatizo ya Juma Kaseja na klabu ya Yanga
yalianza kujionyesha pale ambapo yeye mwenyewe Juma aliona hana
kipaumbele sana kwenye klabu ya Yanga, na hii ni kutokana na yeye
kutokutumiwa kwenye michezo mingi tuliyokuwa tukiicheza sisi tofauti na
zamani ambavyo watu walikuwa wakimuelewa Juma Kaseja ndio golikipa
nambari moja Tanzania”, alisema Muro.
Aliongeza :”lakini kwa mabadiliko ambayo klabu
ilikuwa ikiyapitia nyakati kwa nyakati na kwa mahitaji ya timu kwa
wakati huu tulionao, yapo mabadiliko yamefanyika na yapo maboresho
yamefanyika, mabadiliko ambayo kwa kiasi kimoja au kingine hakikuweza
labda kumfurahisha Juma Kaseja yeye mwenyewe”.
Pia Muro ametolea ufafanuzi kuhusu suala zima la malipo na
makubaliano mengine kati ya Kaseja na Yanga kufuatia golikipa huyo
kuacha kushiriki katika mazoezi na timu hiyo.
”Sisi kwetu hufanyi mazoezi hulipwi, hata kama
unamikataba, naomba nifafanue bila kupepesa macho, hata kama
unamkataba…. safari hii hufanyi mazoezi, huna sababu ya kutofanya
mazoezi, huna ripoti ya mwalimu, huna ripoti ya daktari wa timu, hatujui
kuhusu mambo ya kwako kwenye familia, huji tuu kwenye mazoezi,
..hulipwi chochote na hatutalipa”, alisema Jerry Muro
JERRY MURO AZUNGUMZIA MUSTAKHABALI WA KASEJA NA YANGA
Reviewed by crispaseve
on
23:40
Rating:

Post a Comment