PRODUCER MAN WALTER KUANZA KUTOZA MILIONI MOJA KWA NYIMBO MOJA

Man Walter
Mtayarishaji mahiri wa muziki hapa Bongo, Man Walter
ametangaza kupandisha gharama za kurekodi nyimbo katika studio zake za
Combination Sound kutoka gharama alizokuwa akitoza hapo awali hadi
kufikia shilingi milioni moja.
Man Walter amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba
siku zimezidi kwenda na bei za kurekodi zimekuwa zile zile huku wao
watayarishaji wakibaki wakiwa wamedumaa wakati wasanii wanafanikiwa
kuliko wao na kudai kuwa hajafanya hivyo kwa sababu ya wivu kwa wasanii
bali ni katika kutaka kupiga hatua nyingine mbele kimaisha..
”Ili ufanikiwe kuna vitu
ambavyo unatakiwa uchukue risk, bila kuogopa nini kitatokea, kama
wasanii hawata kwenda kurekodi kwa sababu bei imepanda ni sawa lakini
yeye anategemea ubora wa kazi anaoufanya kwaiyo anaamini anaweza
kuendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki”, alisema Man Walter
Aliongeza :”soko lolote lenye bidhaa bora na
kama wewe mfanyabiashara unaamini bidhaa yako ina ubora na soko huria
unaweza kuweka bei unayoitaka na mteja anayehitaji bidhaa bora atakuja
tuu kwako. Wasanii watakaokuja na kufikia malipo hayo ya milioni moja
atafanya nao kazi”.
Man Walter ambaye amefanikiwa kutwaa Tuzo za Kili mara mbili
mfululizo kama mtayarishaji bora wa mwaka, anasifika kwa kutengeneza
ngoma kali zinazotokea kuwabamba mashabiki ikiwemo Baadae na Tupogo za
Ommy Dimpoz, Dushelele na Mwana za Ali Kiba na ngoma nyingine kibao.
PRODUCER MAN WALTER KUANZA KUTOZA MILIONI MOJA KWA NYIMBO MOJA
Reviewed by crispaseve
on
23:33
Rating:

Post a Comment