RICK ROSS AONYESHA MAPENZI KWA MIAMI HEAT BAADA YA KUCHORA TATTOO HII
Rapa na C.E.O wa lebo ya Maybach Music Group, Rick Ross
ameonyesha mapenzi ya hali ya juu kwa timu ya mpira wa kikapu ya Miami
Heat inayoshirki ligi kuu ya NBA baada ya kuchora tattoo mpya usoni
kwake yenye nembo ya timu hiyo.

Rick Ross akionyesha Tattoo mbili mpya ambazo amechora usoni ikiwemo nembo ya Miami Heat na Dream Chasers ‘DC’.
Rick Ross alikuwa ameongozana na lebo mate wake Meek Mill
ambaye pia alichora nembo ya MMG kwenye kiganja cha mkono wake zoezi
lililofanywa na duka la Unroyal Ink ambao ni wataalam wa uchoraji
Tattoo.
Mapema katika msimu mpya wa ligi ya NBA, Ross alifanya
uwekezaji mwingine mkubwa katika timu ya Miami baada ya kuiwekea dola
10,000 za kimarekani kama sehemu ya kuitabiria kumaliza msimu na rekodi
nzuri kuliko Cleveland Cavaliers, kufuatia Lebron James kuhamia kwenye
timu iyo akitokea kwao.

Rick Ross akichorwa tattoo huku mkononi akiwa ameshika sigara kubwa

Rozzay akionyesha Tattoo nyingine alizochora hapo awali

Meek Mill akionyesha Tattoo ya MMG ambayo amechora kwenye kiganja cha mkono wake

Meek
Mill na Rick Rozzay wakiwa wameunganisha mikono yao ikiwa ni ishara ya
kusapotiana kwa kuchora Tattoo yenye logo ya mwenzake – MMG na DC for
Life.
RICK ROSS AONYESHA MAPENZI KWA MIAMI HEAT BAADA YA KUCHORA TATTOO HII
Reviewed by crispaseve
on
23:29
Rating:

Post a Comment