MAN CITY YAMUONGEZEA MKATABA FRANK LAMPARD HADI MWISHO WA MSIMU

Hatimaye Klabu ya Manchester City imemuongezea mkataba kiungo mkongwe Frank Lampard hadi mwisho wa msimu wa ligi kuu.
Lampard mwenye miaka 36 amemaliza mkataba wake na klabu ya
New York City ya Marekani usiku wa kuamikia leo kwa maana iyo atabakia
Etihad hadi mwisho wa msimu na atakosa mechi za mwanzo za ligi kuu ya
Marekani ‘Major League’ au MLS.
Klabu ya New York City ilimsaini Lampard mara baada ya
kuachwa na Chelsea ya England Juni mwaka jana na klabu ya Manchester
City kumuomba kurejea ili acheze kwa mkopo kwa kuwa ligi ya marekani
inaanza March mwaka huu.
Kuongezewa mkataba kwa Lampard kumekuwa ni faraja kubwa kwa
kocha Emmanuel Pellegrini kwa kuwa atakuwa mbadala wa kiungo Yaya Toure
anayejiunga na timu yake ya Taifa Ivory Coast kuanzia January, 05 katika
fainali za Afrika nchini Guinnea ya ‘GuinneEquator.
Lampard amekishwa ichezea Manchester City mechi 17 akiwa
ameweka wavuni mabao 6 huku akitajwa kuwepo katika kikosi cha leo
kitakachovaana na timu ya Sunderland kwenye uwanja wa Etihad.
MAN CITY YAMUONGEZEA MKATABA FRANK LAMPARD HADI MWISHO WA MSIMU
Reviewed by crispaseve
on
23:00
Rating:

Post a Comment