MAYWEATHER, PACQUIAO WAKUTANA USO KWA USO NA KUSALIMIANA
Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wameudhihirishia
ulimwengu kuwa uhasama uliopo kati yao ni wa ulingoni na sio sehemu
nyingine, hiyo ni baada ya kukutana uso kwa uso na kusalimiana kama vile
sio mahasimu wakubwa.
Mabondia hao wanaoshikilia mataji makubwa ya ndondi,
walikutana katika uwanja wa American Airlines usiku wa kuamkia
leo(Jan27) wakati wa mchezo kati ya timu ya mpira ya Miami Heat na
Milwaukee Bucks katika mchezo uliomaliza kwa Bucks kushinda kwa jumla ya
vikapu 109 – 102 dhidi ya Heat.
Mbali na mchezo huo, mashabiki na wapenzi wa masumbwi Duniani
kote wamekuwa wakisubira kwa hamu mpambano wa wawili hao ambao wamekuwa
wakitambiana kwa kipindi kirefu unaotajwa kufanyika mwezi Mei mwaka
huu. Watazame hapo chini wakisalimiana
MAYWEATHER, PACQUIAO WAKUTANA USO KWA USO NA KUSALIMIANA
Reviewed by crispaseve
on
01:36
Rating:
Post a Comment